Kujifunza Kujifunza ni Stadi Mama ya Stadi Zote
Picha kutoka tovuti ya campaignforlearning Tamko na 3.1.3 la Sera ya Elimu na Mafunzo, 2014 linaweka bayana kuwa elimu ya msingi ni ya lazima na inaishia kidato cha Nne. Tamko 3.1.5 linasisitiza pia kuwa, elimu hii katika mfumo wa umma itatolewa bure. Hizi ni nia njema kabisa na za kupongezwa. Si haba kuwa, hadi sasa utekelezaji wake unafanyika. Hata kama ni kwa taratibu au usio wa kiwango cha kuridhisha. Swali (pengine la msingi) la kujiuliza ni kuwa, elimu hii ya msingi inatoa msingi kweli kweli na je Sera inaeleza bayana msingi unaopaswa kutolewa? Sera inaweka bayana matarajio ya ubora wa elimu na mafunzo kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Kwamba, elimu na mafunzo yatakayotolewa yawe ni ya “ viwango vya ubora unaotambulika kikanda na kimataifa na kukidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa ” (uk 24). Mwanafunzi kutoka katika elimu yenye viwango na ubora unaozungumzwa hapo juu awe na sifa zipi? Sera ya Elimu na Mafunzo, 2014 imeweka bayana k...