Posts

Showing posts from June, 2011

Pengine haikuwa busara kuwafukuza; labda harakati za kutafuta haki na usawa wa binadamu.

Tanzania tunakaribia kuadhimisha miaka hamsini ya Uhuru. Lakini kwa hali duni ya kiuchumi na kisiasa ilivyo, haitamnyima raia wa kwaida kabisa kuamini kuwa uhuru hauna maana kwake. Tazama vita kati ya wananchi na wawekezaji (wakoloni wa kizungu wa karne ya leo) unavyogharimu maisha ya watanzania. Umeme umekuwa ni tatizo sugu ambalo linaweza kutatulika. Waandishi wa habari wanakosa uhuru wao wa kufanya kazi. Haishangazi sana kwa wafanyakazi wa umma kufanya kazi nusu mwaka, mwaka mzima na hadi miaka bila kulipwa stahiki zao ikiwemo mishahara yao. Huu ni utumwa. Inaashiria kuwa bado tuna haja ya kuutafuta uhuru ambao tunadhani tayari tunauogelea.
Hali ya utumwa unaoendelea Tanzania unanifanya niamini kuwa, kwa kuwafukuza wakoloni wa kizungu haikumaanisha kuwa tulipata uhuru na hivyo tukawa huru. Nadhani tulipaswa kutambua tu kuwa, waafrika asili yetu ni Afrika na ili tuwe huru hakukuwa na umuhimu wa sisi (waafrika) kuishi peke yetu(kujitenga) kama ishara ya kuwa huru. Hata hivyo jambo h…

Labda B.W Botha alitumia tafsida.

P.W Botha alikuwa ni raisi wa zamani wa Afrika ya Kusini wakati nchi hii ilipokuwa inatawaliwa. Kuna wakati Raisi huyu alilihutubia baraza lake la mawaziri na nakala ya hotuba yake iliandikwa katika gazeti la Sunday times la Afrika Kusini na David G. Mailu tarehe 18 August 1985.

Botha aliongea mengi yaliyoonekana kuwakashifu waafrika. Miongoni mwa mambo aliyoyayongelea ilikuwa ni hili: "By now everyone of us has been seen it practically that Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other".
Naam, hadi sasa, nchi zote za Afrika hazitawaliwi tena na wakoloni wa kutokanchi za ng'ambo; tulishapata uhuru wa kujioongoza kama sio kujitawala. Hali halisi inaonesha tunashindwa kutumia vizuri ule uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe; uhuru ambao tuliutafuta wenyewe kwa kumwaga damu ilipobidi. Najaribu kutafakari kuhusu Afrika ya sasa. Hakuna dalili iliyowazi kweli kuwa waafrika hatuwezi kujiongoza (kidemokrasia)kama alivyosema ndugu Botha miaka kadhaa …