Posts

Showing posts from March, 2017

Walimu, Ninyi ndio Mnaojifunza, Wanafunzi wenu ni Wapokea Taarifa tu

Image

Mbinu za Kusaidia Kujenga Utamaduni wa Ufundishaji wa Kiudadisi Mashuleni

Image

Ufundishaji wa Kiudadisi: Maana, Faida na Namna Unavyoweza Kutumiwa

Image
Picha kwa hisani ya UNESCO learning Portal

Matumizi ya njia ya ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi umeenea maeneo mbalimbali duniani na hususani katika nchi za Ulaya. Ufundishaji Unaomzingatia Mwanafunzi ni mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji unaompa mwanafunzi fursa ya kujibidisha ili kujipatia maarifa na kutumia maarifa yake ya awali katika kujenga maarifa mapya badala ya kuwa mpokeaji wa maarifa na kisha kuyatumia kwa namna ya kuyakariri.
Katika machapisho mbalimbali, Ufundishaji Unaomzingatia Mwanafunzi umekuwa ukipewa majina anuai kama vile ufundishaji shirikishi, ufundishaji unaomzingatia mtoto, ufundishaji wa Kiudadisi na majina mengine. Hata hivyo, watumiaji wengi wa mfumo huu wa kufundishia na kujifunzia wanatumia zaidi istilahi ya Ufundishaji wa Kiudadisi.
Ufundishaji wa Kiudadisi bila shaka ni istilahi pendwa kwa kuwa inasadifu moja ya tabia muhimu ya udadisi anayopaswa kuwa nayo mwanafunzi wakati wa ujifunzaji wake na hata kat…