Posts

Showing posts from November, 2010

Kiswahili na Kiingereza; Twazitaka lugha hizi kwa pupa, na tunazikosa zote.

Kiswahili ni lugha kuu ya mawasiliano kwa watanzania na ndio maana inatambulika pia kama lugha ya Taifa. Kiingereza ni lugha rasmi ambayo hutumika maofisini na mashuleni, hususani shule za upili hadi vyuo vikuu. Hutumika kama lugha ya kufundishia na mawasiliano mengine.

Kinyume na matarajio, sehemu ambazo kiingereza kilipaswa kutumika, maofisini na shuleni, hakitumiki ipasavyo, bali kiswahili ndicho kinachoshika hatamu.

Mbali na kutoitumia lugha ya kiingereza mashuleni na kwenye ofisi, nje ya maeneo haya hali ni hiyo hiyo, watu wanatumika kiswahili kwa uhuru wao kwani ndiyo lugha pekee ituunganishayo watanzania bila kujali sana elimu aliyonayo mtu. Wapo watanzania wachache wasiokijua kiswahili vizuri kwa sababu wamekuwa wakitumia lugha za makabila yao kiasi cha kukisahau kiswahili lakini asilimia kubwa tunakizungumza vizuri. Mashuleni, walimu wanawahimiza wanafunzi wao kutumia kiingereza hata wawapo majumbani kwao kama namna ya kuijua zaidi lugha hii. Kwa mantiki hii, kiswahili kinapew…

Jamii yangu; kijijini Siuyu.

Image
Kizazi cha sasa na upotezaji wa muda usio na tija yoyote.Asubuhi ya leo vijana wakijiburudisha na pool table.


Wazee nao asubuhi hiyo hiyo wakicheza bao.

Kwenye makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema "NIPO SINGIDA" nilieleza kushangazwa na hali ya vijana na wazee kuonekana asubuhi wakicheza bao na pool table. Hali ndio kama muionayo pichani.

Sehemu hii ni maarufu kidogo. Pamechangamka kwa kiasi, panaitwa "madukani" kwani ni sehemu yenye maduka kadhaa yanayohesabika lakini.

Cha ajabu kabisa pamoja na uwepo wa maduka haya, hukuna duka liuzalo "mikate". Nakumbuka siku nilihitaji mkate na nilitembelea maduka yote bila mafanikio kama vile nilikuwa na mpango wa kuwasalimia wauzaji.

Ni kweli kuwa mikate hiyo ikiwepo haitanunuliwa? Ingenunuliwa, na mimi ningekuwa miongoni mwao. Tatizo watu hawana elimu ya ujasiriamali. Vijana hawasomi majira ya wakati. Hawaumizi kichwa. Utaratibu ni ule wa bora kumekucha, nimepata ugali mlenda mchana, usiku ugali chu…

Baraza la mitihani la Taifa (NECTA), umakini zaidi watakiwa.

Image
Wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao kunaweza kuchangiwa na mambo mengi. Wengi tujuavyo au tuzanivyo; mwanafunzi akifeli mitihani hususani ile ya taifa, tunachukulia kuwa ni uzembe wake kwani hakuzingatia vyema masomo au uwezo wake darasani ni mdogo. Ndivo ambavyo wazazi/walezi hata na walimu wengi wajuavyo.

Kweli, hizi zaweza kuwa ni sababu lakini zipo sababu nyingine ambazo watu wengi huwa hawazidhanii kuwa zaweza kusabisha mwanafunzi kufeli.

Leo nina nia moja tu ya kuzungumzia uzembe ujitokezao mara kwa mara katika mitihani ya taifa, yani ile ya kumaliza shule ya msingi na sekondari(kidato cha nne na cha sita). Uzembe niuongeleao ni huu wa kukosewa kwa baadhi ya maswali ya mitihani ya taifa inayosimamiwa na baraza la mitihani la taifa.

Mitihani hii pamoja na umuhimu wake kwa watahiniwa( kwani ndio inayoamua mustakabali wa watanzania wengi kimasomo na kimaisha kwa wale waliopata bahati ya kusoma na wale waliopata bahati ya kusomesha), imekuwa ikija na makosa mbali m…