Posts

Showing posts from March, 2010

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"

Image
Umewahi kuusikia au kuuona mmea uitwao Mlonge? Au kwa lugha ya kilatini "Moringa Oleivera"? Binafsi niliwahi tu kuusikia na kwa bahati nzuri hivi majuzi nilibahatika kuuona. Mmea unaoonekana pichani wenye shina kubwa ndio Mlonge wenyewe kwa mujibu wa aliyenionyesha kwani mimi sikuwahi kuuona kabla.

Mmea huu ni dawa na unaaminika kutibu magonjwa mengi yawasumbuayo binadamu pengine hata na wanyama wengine. Majani yake,matunda yake,magome yake,maua na mizizi hutumika kama dawa, kila sehemu ya mti kwa umuhimu wake.

Inasemekana matunda yake yanatumika kama mboga kwa kukatakata kama kabichi na majani yake pia hutumiwa kama mboga kwa kupika kama mchicha. Majani yake hutibu magonjwa mbalimbali na kuongeza virutubisho vya mwili.

Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment).

Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai m…

Matatizo ndani ya ndoa Vs Matatizo ya ndoa.

Image
Kwa miaka ya sasa maisha ya ndoa yamekuwa ni ya siri kubwa na vijana wamekuwa wakiingia ktk maisha haya bila uelewa mzuri na wa kutosha. "Ambao hawajaingia katika maisha ya ndoa wanatamani kuingia na wale walio ndani ya ndoa wanatamani kutoka". Kwa bahati mbaya sana mafunzo ya jando na unyago kwa jamii ya sasa hayapo,na kama yapo ni kwa sehemu ndogo kabisa ya jamii. Hivyo vijana wengi wanaingia ktk maisha haya bila uewelewa wa kutosha na wanajikuta wanakabiliana na changamoto ambazo hawakuzitegemea. Binafsi nimeshawishika kujiuliza ni kwa nini wanandoa wanaishia tu kuwaambia vijana kuwa wanatamani kutoka ktk ulimwengu wa maisha ya ndoa, ni vile tu maji yameshayavulia nguo hivyo ni sharti wayaoge. Nilibahatika kukaa na wanandoa kadhaa ili kutaka kujua huwa wana maana gani pale wasemapo wanatamani kutoka ktk maisha ya ndoa ilihali vijana tuna mcheche wa kuingia huko tena kwa kujiamini. Katika kuvinjari akili kadhaa za wanandoa,nilipata kujuzwa mambo makuu mawili; "m…

Chemsha bongo

Utachukua uamuzi gani pale mlinzi wako wa usiku anapokusimulia ndoto aliyoota usiku wa leo na anakutaka uahirishe safari yako kwani safari yako kulingana na ndoto yake inaonyesha basi utakalosafiria litapata ajali na watu wote watapoteza maisha? Fikiria kuwa umeahirisha safari na kweli ajali ikatokea,kwa maana kuwa ameokoa maisha yako. Utamfukuza kazi au utaendelea kuwa naye?