Posts

Showing posts from September, 2012

Tanzania Iliyobarikiwa Isiyo ya Wabarikiwa

Image
Picha ya Muonekano wa Kaldera ya Ngorongoro Tanzania inajulikana kuwa na rasilimali nyingi sana ambazo kama zingetumika vizuri, basi watanzania tungekuwa katika hali nafuu sana ya maisha kuliko hivi sasa. sitamani kuwakumbusha utajiri ambao nchi ya Tanzania ilionao kwani umeshakuwa ni wimbo ambao kwa sasa pengine hakuna tena anayetaka kuusikiliza kabisa. Kama nilivyotangulia kusema katika bandiko lililopita, nilipata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya mkoa wa Singida, hususani wilaya ya Iramba. nilisema pia, kuna mengi niliyojifunza kwa kusimuliwa na kwa kujionea mwenyewe. leo nitawajuza kuhusu mgodi mpya wa dhahabu nilioushuhudia katika ukanda wa bonde la ufa la sekenke katika eneo liitwalo Mgongo. Mgodi wa Mgongo uko wilaya ya Iramba-sekenke, kama mita mia mbili kutoka ilipo shule ya msingi  Mgongo; shule ambayo ndiyo niliyofikia kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya waalimu walio katika mafunzo ya muda mrefu ya kufundisha. Nilifika hapo tarehe 07/03/2012 na nilipewa taarifa ku

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?