Posts

Showing posts from July, 2010

Mashaka ya namna Malaria isivyokubalika.

Asilimia kubwa kabisa ya vita dhidi ya malaria imeelekezwa kwenye matumizi ya vyandarua vyenye ngao.

Hivi kila mmoja akitumia chandarua chenye dawa ya ngao, ni kweli kuwa malaria itakuwa imeshadhibitiwa?

Mimi kwa mtizamo wangu nasema hapana.

Kwa kutilia msisitizo wa matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya ngao, kama njia kubwa ya kupambana na malaria, ni ishara au ni kidokezo kuwa kwa asilimia kubwa watu hupata malaria wakiwa wamelala. Kuna ukweli hapa? Sijui kama kuna tafiti yoyote kuhusiana na hili.

Mtu anaweza kuumwa na mbu aenezaye malaria akiwa amekaa chumbani, pembeni mwa kitanda, sebuleni, barazani na mahali popote pale ambapo mbu waenezao malaria wapo. Hii ni kusema kuwa mahala popote mtu anaweza kupata malaria, si wakati akiwa amelala tu! Huu ni ukweli mtupu ambao hata hauhitaji utafiti.

Kwa kulizingatia hili mimi nadhani, vita kubwa ingeelekezwa kwenye kuwaangamiza wadudu hawa huku watu wakisisitizwa kutumia vyandarua vyenye dawa kwa uhakika zaidi. Ila matumizi ya vyandarua vyenye …

Tunazingatia matumizi ya Lazima na Hiari kwa pato letu?

Ni mda mrefu ulipita sikuonekana katika ulimwengu huu wa ku-blogu. Nilibanwa na baadhi ya majukumu, na sasa nimerudi tena na tupo pamoja. Niombe radhi kwa kutokuweka wazi juu ya adimiko langu.Naam, wakati wa adimiko, nilipata kujifunza mengi, na leo naona ni vema nigusie kidogo matumizi ya pato la mtanzania mmoja mmoja na mchango wake katika kuendeleza wimbi la umasikini au kuweza kujikwamua na umasikini.Popote pale Tanzania, mjini na vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi huonekana katika pilikapilika za hapa na pale. Wapo wafanyao kazi halali na wale wasiofanya kazi halali, lakini mwisho wa siku kila mmoja anapata ujira wake.Wapo waliojiajiri na pia walioajiriwa. Waliojiajiri, mwisho wa siku huweka chao kibindoni na wale walioajiriwa husubiri mwisho wa mwezi ndipo waweke chao kibindoni. Maisha haya humgusa yeyote yule ambaye si tegemezi katika familia au sehemu aishiyo.Huko mijini, watu huonekana kila mmoja na pilika yake ilimradi mkono uingie kinywani…