Posts

Showing posts from May, 2009

Tule papai kivingine kabisa.

Papai bichi linaweza kutumika kama mboga.

Twendeni jikoni pamoja. Hata wanaume tunaweza, eti haturuhusiwi kuingia jikoni! Mke akiugua au akisafiri!
Twende pamoja.

1. Chukua mapapai yako mabichi yaliyokomaa ila bado kuiva.

2. Yaoshe, kisha yachonge vizuri halafu uyaoshe tena kwani yatakuwa na utomvu.


3. Yakwangue na kikwaruzio cha karoti, hapo utapata saizi ndogo ndogo kama wakati unapokwaruza karoti. Baada ya hapo, chemsha kwa muda mfupi na maji kidogo, kisha epua.


5. Kaanga kitunguu pembeni kisha weka nyanya kulingana wingi wa mboga zako, pia na karoti kama zipo, acha mchanganyiko huu uive vizuri mpaka kupata rojo ya nyanya.


6.Weka mchemsho wako wa mapapai kisha, changanya vizuri na acha mboga yako iive vizuri, pia usisahau kuweka chumvi kwa kadiri ya kipimo chako.

Kwa wale wanaoweza kupata mapapai, wajaribu kupika mboga hii, ni tamu sana.

Nimtakie kila mmoja atakayesoma hapa wakati mzuri na muwe na furaha kila sekunde ya maisha yenu.

JARIBU UJIONEE.

Wakati wa mchana ukiangalia kivuli chako kwa muda wa kama sekunde kumi hadi ishirini hivi, na kisha bila kuchelewa ukiangalia mawinguni(sky)utakiona kile kivuli chako(mwonekano wake ukiwa ni wa rangi nyeupe) kikiwa kimekuzwa zaidi.Ukiangalia sehemu nyingine mbali na kwenye mawingu hutakiona.


Jaribu ujionee mwenyewe! Sababu hasa ni ipi?

Inawezekana.

Kuchemsha maji kwa kutumia mfuko wa nailoni(plastic material).


1. Chukua mfuko wako wa nailoni, ujaze maji, ikiwezekana kusiwe na hewa yoyote ndani, yani nafasi yote ya mfuko ichukuliwe na maji.

2.Washa moto na tafuta namna ya kushikilia mfuko wako kwenye moto.
Maji yatapata moto bila mfuko huo kuyeyuka au kuungua.
Jaribu!
Pia unaweza kuchemsha maji kwa kutumia chupa yoyote ya plastiki ilimradi uhakikishe hakuna hewa(air bubbles) ndani ya chupa.

Jiulize, kisha nipe jibu.

Katika mihangaiko yako hapa duniani, ni kitu gani hasa unakitafuta?
Je, ni mali nyingi,?
Pesa nyingi?
Au unatafuta tu kuishi na watu vizuri?

Ukipata ajira nzuri, ukajenga nyumba,ukaoa/ ukaolewa, je kuna cha zaidi utakuwa unahitaji?


Mtu akikupa nyumba nzuri tu ya kuishi yenye kila kitu, na akakupa kila unachohitaji, je utaridhika, utajisikia kuwa ulichokuwa unakitafuta umeshakipata? Ukifanya jambo fulani, ni kitu gani huashiria mafanikio?


Katika mihangaiko yako, mwisho wake unategemea nini? Kama ni maisha mazuri, kama ni mshahara mzuri, kama ni pesa, kama ni mali, vyote hivi vinaashiria nini?
Jiulize, kisha nipe jibu.