Tule papai kivingine kabisa.

Papai bichi linaweza kutumika kama mboga.

Twendeni jikoni pamoja. Hata wanaume tunaweza, eti haturuhusiwi kuingia jikoni! Mke akiugua au akisafiri!
Twende pamoja.

1. Chukua mapapai yako mabichi yaliyokomaa ila bado kuiva.

2. Yaoshe, kisha yachonge vizuri halafu uyaoshe tena kwani yatakuwa na utomvu.


3. Yakwangue na kikwaruzio cha karoti, hapo utapata saizi ndogo ndogo kama wakati unapokwaruza karoti. Baada ya hapo, chemsha kwa muda mfupi na maji kidogo, kisha epua.


5. Kaanga kitunguu pembeni kisha weka nyanya kulingana wingi wa mboga zako, pia na karoti kama zipo, acha mchanganyiko huu uive vizuri mpaka kupata rojo ya nyanya.


6.Weka mchemsho wako wa mapapai kisha, changanya vizuri na acha mboga yako iive vizuri, pia usisahau kuweka chumvi kwa kadiri ya kipimo chako.

Kwa wale wanaoweza kupata mapapai, wajaribu kupika mboga hii, ni tamu sana.

Nimtakie kila mmoja atakayesoma hapa wakati mzuri na muwe na furaha kila sekunde ya maisha yenu.

12 comments

Yasinta Ngonyani said...

Asante kwa hii mboga mpya ya papai. Nitakapofika tena huko nyumbani nitajaribu. Kwani huku ni bei sana. Papai moja ni shilingi 3000/=

Kissima said...

Pole sana dada Yasinta, hakika mapapai huko ni ghali sana!
Karibu Moshi huku mapapai bure kabisa.

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana Kissima Itabidi nije huko Moshi. kwani hali ya hewa ya huko itapatani nami na ntakula mapapai mengi.

Kissima said...

Karibu sana dada Yasinta.

mumyhery said...

papai bichi!!! sijui ntalipata wapi jamani, afadhali ungesema la kuiva labda nigepata hata la kopo

Kissima said...

Usihofu dada Mumyhery, siku ukirudi huku nyumbani utaandaa mboga hiyo ya papai.
Nakushukuru kwa kukitembelea kibaraza changu, karibu tena na tena.

Anonymous said...

Jtgt

Mzee wa Changamoto said...

Kwanza nishukuru kwa kututakia wakati mzuri. Ni baraka saana kupata baraka toka kwa watu wema kama wewe.
Pili nashukuru kwa "maungo" haya ambayo nikijaaliwa kulinyaka hilo papai bichi itakuwa "muswano"
Blessings

Serina said...

Nimesoma papai bichi nikafikiria biriani... nami nitajaribu.

Kissima said...

Ni papai bichi dada Serina, ambalo ganda lake halijakuwa la njano,bado la kijani kabisa. Jaribu, halafu utaniambia mboga hiyo jinsi ilivyo nzuri.

Yasinta Ngonyani said...

Kissima upo mzima naona umepotea kweli?

Kissima said...

Mimi sijambo dada Yasinta,mimi mzima wa afya.
Majukumu fulani fulani tu yamenitinga,
lakini tupo pamoja.

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.