Posts

Showing posts from November, 2011

Kutana na MAEMBE AND THE SPIRITS; wakupe CHANJO YA RUSHWA.

Ni ukweli usiopingika kuwa,Tanzania ya sasa inagubikwa na wimbi la WANAHARAKATI wa kila aina kuanzia wa kisiasa, kiuchumi na wale wa kijamii. Kimsingi katika nyanja zote za maisha ya mwananchi wa tanzania, wanaharakati wametokea kuonesha mapambano, na mara nyingi yamekuwa ni ya kujaribu kuzirekebisha taasisi au asasi husika ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zkionesha dalili ama moja kwa moja kuonesha kupindisha haki, kunyima demokrasia, kuzuia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi na matakwa ya watanzania kwa ujumla.


Maembe And The Spirits, ni miongoni mwa wanaharakati walioamua kujitosa katika msitu wenye simba wengi katika harakati za kukabiliana na tatizo sugu la RUSHWA nchini Tanzania na kwingineko duniani. Kikundi hiki, kikiongozwa na bwana Vitali Maembe, kwa kutumia nyimbo mbalimbali wanazotunga wenyewe pamoja na majadiliano ya wazi, kimeamua kwa gharama zao, kutembelea maeneo yote ya Tanzania ili kuwaelimisha watanzania mambo mbalimbali yahusuyo rushwa yak…