Posts

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani? Sehemu ya Pili.

Image
Katika makala iliyotangulia, nilijadili mambo makuu mawili ambayo walimu na wanafunzi wanapaswa kuyafanya ili kuendana na mfumo wa ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi. Mamo haya mawili ni wajibu wa mwalimu na mwanafunzi na malengo ya maudhui yanayofundishwa.

Makala haya yanalenga kuendelea kujadili namna nyingine tatu zinazoweza kuzingatiwa na walimu na wanafunzi ili kufanikisha utekelezaji wa mitaala inayomzingatia mwanafunzi. Kwenye makala haya, tutaaangalia wajibu wa kujifunza, nafasi ya mwalimu na mwanafunzi kuhusu masuala ya ujifunzaji na malengo ya upimaji wa mwanafunzi.

Wajibu wa Kujifunza.  Wajibu wa kujifunza ni hali ya utayari wa mwanafunzi kushiriki kwenye mchakato wa ujifunzaji bila kulazimishwa ama kushurutishwa. Hali ilivyo sasa, wanafunzi wanafahamu wajibu wa mwalimu ni kuleta maarifa darasani na wajibu wa wanafunzi ni kumsikiliza mwalimu na kuandika nukuu. 
Katika mfumo huu, mwalimu ndiye anayehangaika kujifunza kisha anakuja darasani kufafanua kile alichojifunza. Huu…

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?

Image
Picha: Mwandishi wa makala
Kama mnakumbuka, kati ya mwaka 2005 na  2007 yalitokea mabadiliko ya mitaala, hususani kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu. Kulikuwa na msemo uliovuma sana wa "muhamo wa ruwaza" au "paradigm shift" kwa kiingereza.

Ruwaza ni mfumo au imani inayomuwezesha mtu kutekeleza jambo fulani kulingana na matakwa na taratibu fulani zinazofahamika. Kwenye ufundishaji, iliaminika kuwa mitaala yetu ilikuwa ya mfumo unaomuona mwalimu kama chanzo cha maarifa na mwanafunzi kama pipa linalosubiri kujazwa tu maarifa.

Mitaala mipya inaaminika kuwa ya ruwaza tofauti, ndio maana mabadiliko haya yakaitwa ya kuhama kwa ruwaza. Namna mitaala ilivyoandikwa na namna ya kuitekeleza ni miongoni mwa mabadiliko haya. Kwa mfano, mabadiliko haya yalipelekea maandalio ya masomo yawe na kipengele cha upimaji kwa kila hatua ya somo. Pia, zimependekezwa njia na mbinu anuai za kufundishia na kujifunzia zinazoakisi mabadiliko haya.

Hata hivyo, tafiti nyingi zina…

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili

Image
Hakuna mjadala kuwa upimaji endelevu ni sehemu muhimu sana wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Taarifa za namna ufundishaji na ujifunzaji unavyokwenda zinategemewa kupatikana kupitia upimaji endelevu bora.

Makala haya yanalenga kuendelea kujadili mambo makuu manne kama tulivyoyaona katika makala iliyotangulia. Mambo hayo ni ufafanuzi wa kina wa mambo makuu yanayopaswa kujifunzwa na wanafunzi (clarifying learning), kuwajengea wanafunzi ari ya kujifunza (activating learners), kutoa mrejesho wa maendeleo yao (providing feedback) na kutafuta ushahidi wa ujifunzaji (eliciting evidence of learning).

Katika makala haya nitajadili utoaji wa mrejesho wa Shughuli za Ujifunzaji (providing feedback) na utafutaji wa ushahidi wa ujifunzaji (Eliciting evidence of learning).

Kutoa Mrejesho wa Shughuli za Wanafunzi (Providing Feedback) Kila anachokifanya mwanafunzi, anatamani sana kupata mrejesho wa usahihi wa anachokifanya. Hivyo, kutoa mrejesho wa yale wanayoyafanya wanafunzi darasani ni …

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Image
Upimaji endelevu wa mwanafunzi ndio namna pekee ya kutoa taarifa za maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi katika kufikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa kwake. Kwa hiyo, upimaji endelevu ni shuhguli ya msingi mno ya kuzingatiwa na mwalimu na wanafunzi. 
Upimaji endelevu siyo shughuli ya mwalimu peke yake. Ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na manafunzi. Hii ni kusema kuwa, upimaji endelevu ni sehemu ya ujifunzaji wa mwanafunzi na ufundishaji wa mwalimu. Ikiwa tunahitaji kuona upimaji wenye tija, basi kila mmoja ni lazima atimize wajibu wake kwa kushirikiana.
NWEA katika chapisho lao la mwaka 2016 linaloelezea mambo makuu manne ya kuzingatia ili kuleta ufanisi kwenye upimaji endelevu, wanaeleza kuwa upimaji endelevu ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na wanafunzi wa kukusanya ushahidi wa ujifunzaji wa wanafunzi kwa lengo la kuboresha kile kinachoendelea darasani, kwa maana ya mchakato wa ujifunzaji wa wanafunzi.
Ili kufanya mchakato wa upimaji endelevu kuwa wa mafanikio, wana…

Walimu na Teknolojia: Zifahamu Tovuti Nzuri kwa Ajili ya Walimu

Image
Katika makala kadhaa kwenye blogu hii, nimekuwa nikijadili kuhusu namna teknolojia zinavyoweza kutumiwa kwenye ufundishaji na ujifunzaji. Pamoja na changamoto nyingi katika mazingira ya kufundishia, bado ninaamini kuwa, matumizi ya TEHAMA kwenye ufundihsaji ni moja ya suluhisho la changamoto kadhaa za ufundishaji na ujifunzaji. Moja ya matatizo yanayoweza kutatuliwa na TEHAMA ni upungufu wa zana za kujifunzia kama vile vitabu na vyanzo vingine kama vile videos, picha, games na animations.

Kutokana na uwepo wa namna mbalimbali za watu kujifunza, nimeona nitenge muda kidogo wa kuandaa video zinazoelezea tovutinzuri kwa ajili ya walimu na wanafunzi. Ninaamini kuwa video hizi zitakuwa hamasa kwa walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanaopenda kujifunza namna mbalimbali wnavyoweza kutumia teknolojia kwenye ujifunzaji.

Ninaamini pia kuwa, hii ni hamasa kwa wale wasiopenda kusoma maandiko bali kujifunza kwa kutazama ama kufuatilia videos.

Katika makala haya, ninaitambulisha kwako Youtube…

Classroom Assessment in Learner Centered Pedagogy

In learner centered pedagogy, teaching approaches have changed. Teachers are facilitators of learning and students are experts who interact extensively with available resources to build on their knowledge, skills, and understanding of the subject matter. 
In learner centered pedagogy, classrooms should be viewed as “Workshops” and students as experts who interact with available tools (learning resources) to produce desired products (achieving learning outcomes). One of the potential role of teachers/ facilitators in these workshops is to ensure all the necessary tools (learning resources) are available or arranging effective use of few available resources. 
To be clear in the issue of availability of learning resources, I don’t believe in the “lack of sufficient resources” saying. I believe in the idea of using the only few available or a single resource available in a meaningful way. I remember my little thinking;
It is far very helpful for a teacher who think of a way to share the only…

Understand Four Purposes of any Educational Assessment Process