Posts

Showing posts from September, 2014

Utaratibu Huu wa Kuoa/Olewa ni Mzuri, Unahitaji Kuboreshwa Kidogo.

Image

Moja ya Matatizo Yanayoikumba Sekta ya Elimu ni Kukosekana kwa Uwajibikaji.

Image
Vyoo vya kutegemewa katika moja ya shule za sekondari hapa Tanzania Madhara ya kukosekana kwa uwajibikaji
Uwajibikaji ni moja ya dalili kuu ya Uzalendo. Mtu aliye na sifa ya uzalendo, lazima awe muwajibikaji. Sekta nyingi hapa Tanzania zinashindwa kupiga maendeleo yenye tija kwa sababu mbalimbali, mojawapo na iliyo kuu ni kukosekana kwa uwajibikaji. Lengo la makala hii, ni kujadili viashiria kadhaa vya kukosekana kwa uwajibikaji na uwajibishwaji katika sekta ya elimu nchini Tanzania. Wadau wote wa elimu kuanzia serikali na mamlaka zake husika, wakuu wa shule, walimu, wazazi/walezi, jamii na wanafunzi wenyewe wnahusika katika suala la uwajibikaji. Kila kundi lina nafasi yake na wajibu wake katika kufikia malengo yaliyokusudiwa. Muhusika wa kwanza anayepaswa kuwajibika ni mwanafunzi mwenyewe. Kuna ule msemo usemao, “unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini siyo kunywa maji”. Shule inaweza kuwa na mazingira rafiki ya kusomea, walimu wa kutosha na walio na vigezo, wawajibikaji …

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Image
Umbali kati ya shule na waishipo wanafunzi, hususani kwa shule za kutwa, umebainishwa na watafiti wa elimu kuwa unaathiri masomo ya mwanafunzi. Picha kutoka Fullshangwe Blog. Imetumiwa bila ruhusa.


Kama nilivyodokeza katika makala iliyotangulia, makala hii inajadili mambo kadhaa ya msingi ya kuzingatia ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa shule, hususani za msingi na sekondari. Mambo haya ni matokeo ya tafiti mbalimbali za masuala ya uboreshaji na ufanisi wa shule. Ubora wa elimu Tanzania umeendelea kushuka siku hadi siku, na mikakati kadhaa ikiwamo ya matokeo makubwa sasa imeanzishwa katika kukabiliana na changamoto hii.. Harakati yoyote ya kuboresha ufanisi na ubora wa shule hauna budi kuzingatia mambo kadhaa yakiwemo haya takayoyajadili hivi punde kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kielimu.

Tunawezaje Kuongeza Ufanisi na Ubora wa shule? Watafiti wa Masuala ya Ubora na Ufanisi wa Shule Wanatujuza.

Image