Posts

Showing posts from February, 2011

Tumkaribishe Mshairi

Ulimwengu wa kublogu unazidi kushika kasi hasa hasa katika kipindi hiki ambacho huduma ya intaneti inavyozidi kupatikana kwa urahisi. Ni jambo la kujivunia kuwa kila siku watu wanazidi kujumuika katika kuielimisha jamii kwa njia ya mtandao na hususani kwa njia hii ya magazeti huru ya mtandaoni, na kila mmoja kwa namna yake aonavyo inafaa.

Basi, leo hii naomba kumtambulisha ndugu David Mgaya ambaye naye kwa kupitia mashairi, ameona analo jambo la kutuelimisha wanajamii. Ndio kwanza anaanza, lakini ni imani yetu kuwa anayo mengi ya kutufunza na kutuburudisha. Waweza kubofya hapa ili upate kuona kile akusudiacho kujifunza nasi.
Karibu sana ndugu Mgaya.

Soko la Magulioni-Singida Mashariki

Image
Kati ya sehemu ambazo wananchi wake wanahatarisha maisha yao, basi ni hapa katika soko hili liitwalo MAGULIONI ambalo lipo eneo maarufu liitwalo Njia panda ya Makiungu pembezoni mwa barabara ya Singida-Manyara. soko hili huwa kila siku ya Jumamosi na husheheni vitu vya kila aina kuanzia mboga mboga, nguo, kuku, miwa, vyungu, vyakula mbali mbali vikiwemo viazi vitamu vilivyopikwa na ambavvo havijapikwa, majembe n.k Kiujumla, halitofautiani na masoko mengine ambayo ulishawahi kuyaona.

Mbali na upatikanaji wa vitu mbali mbali nilivyojitahidi kuvitaja, lakini pia, kila Jumamosi idadi kubwa ya watu hulitegemea sana soko hili kwa kitoweo cha nyama: kuanzia ya ng'ombe hadi ya mbuzi. Walaji wa nyama hizi kwa hakika wapo katika hatari kubwa sana kwani kulingana na uchunguzi wangu niligundua kuwa hakuna dakitari wa kuangalia uhalali wa matumizi ya nyama hizo, machinjio duni na pia sehemu za kuuzia nyama hizo ni hatari kabisa kwa afya za walaji.

Picha hapa chini zinaonesha baadhi ya mabucha …

Miaka mitano baadae..

Image
Sehemu ya juu ya kitabu kipya cha kufundishia
cha hisabati kidato cha tatu.

Ni takribani miaka matano sasa imepita tangu serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi irekebishe mtaala wa masomo kwa shule za sekondari, kidato cha KWANZA hadi cha NNE. Kwa miaka yote hii mitano hakukuwa na vitabu vya rejea vinavyoendana na mtaala huu vilivyotolewa na Wizara.

Hatimaye sasa baada ya miaka hiyo mitano , serikali imewakumbuka wawezesha wanafunzi kupata maarifa (Waalimu) kwa kuwapatia vitabu hivi. Binafsi naishukuru wizara kwa jambo hili jema japokuwa limekuja kwa kumchelewa.

Labda watu wanaweza kujiuliza kwa kipindi chote hiki cha miaka mitano, walimu wamekuwa wakitumia vitabu gani katika fundisha. Watu binafsi walitumia nafasi hii vyema kuandaa vitabu ambavyo walihakikisha vinahusisha mada zote zilizobainishwa kwenye mtaala huu uitwao mpya.

Binafsi nimekuwa nikifundisha somo la hisabati na nimekuwa n…