Posts

Showing posts from May, 2012

Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?

Sifa ya mwanafunzi anayetaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa sasa ni kuwa mbali na mambo mengine, lakini ni lazima awe na ufaulu usiopungua alama 27 daraja la IV . Kwa upande wa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada, ni lazima wawe na ufaulu wa subsidiary moja na principal pass moja kwa masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari. Vikomo hivi kwa hakika ni vya hali ya chini sana hususani kwa watu wanaotarajiwa kupewa jukumu la kufundisha. Serekali imeridhika na inalifumbia macho jambo hili kila uchao. Baada ya matokeo ya kidato cha nne, nafasi zinazotangulia kutolewa ni zile za wanafunzi watakaoendelea na masomo ya sekondari ya kidato cha tano na cha sita na wale wa chuo cha usimamizi wa maji. Wanafunzi wanaopata nafasi hizi ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu . Baada ya hapo, nafasi za ualimu hutangazwa ili waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya ngazi za juu, waombe. Mara nyingi hawa huwa ni wale wenye u

Nimepata nafasi; ninaitumia vizuri.

Nimepata nafasi; ninaitumia vizuri Ni dhahiri shahiri kuwa watanzania wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitabu. Kusoma vitabu ni tabia na wengi wetu hatuna tabia hii. Ila jambo la kutia moyo ni kuwa watu tuna uwezo wa kubadili tabia endapo tutakuwa na moyo wa kufanya hivyo. Mimi sikuwa na tabia ya kusoma vitabu, lakini nimejizoesha na sasa angalau kusoma vitabu pamoja na kuwa, kasi sio kubwa sana. Nimepata bahati ya kuwa mwalimu wa kuwaandaa walimu wa shule za msingi. Jukumu hili ni nyeti sana pamoja na kuwa serikali ya Tanzania haitambui umuhimu wa walimu hawa wa shule za msingi. Mazingira ya kufundishia bado ni magumu yenye kukatisha tamaa kabisa. Bila shaka, ni walimu wachache sana wenye (angalao) kuridhika na mazingira ya kazi yao ya kufundisha. Pamoja na ugumu wa kazi, lakini nimejitwika jukumu, jukumu la kuwajengea tabia na kuwakumbusha walimu watarajiwa umuhimu wa kusoma vitabu. Ninatambua nafasi waliyonayo walimu hawa wa shule za msingi katika kuk

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?