Posts

Showing posts from September, 2017

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili

Image
Mambo makuu ya kuzingatia ili kufanikisha upimaji endelevu wenye tija. Picha: Mwandishi wa Makala. Hakuna mjadala kuwa upimaji endelevu ni sehemu muhimu sana wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Taarifa za namna ufundishaji na ujifunzaji unavyokwenda zinategemewa kupatikana kupitia upimaji endelevu bora. Makala haya yanalenga kuendelea kujadili mambo makuu manne kama tulivyoyaona katika makala iliyotangulia. Mambo hayo ni ufafanuzi wa kina wa mambo makuu yanayopaswa kujifunzwa na wanafunzi (clarifying learning), kuwajengea wanafunzi ari ya kujifunza (activating learners), kutoa mrejesho wa maendeleo yao (providing feedback) na kutafuta ushahidi wa ujifunzaji (eliciting evidence of learning). Katika makala haya nitajadili utoaji wa mrejesho wa Shughuli za Ujifunzaji (providing feedback) na utafutaji wa ushahidi wa ujifunzaji (Eliciting evidence of learning). Kutoa Mrejesho wa Shughuli za Wanafunzi (Providing Feedback) Kila anachokifanya mwanafunzi, anatamani sana

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Image
Picha: Blogger. Upimaji endelevu wa mwanafunzi ndio namna pekee ya kutoa taarifa za maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi katika kufikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa kwake. Kwa hiyo, upimaji endelevu ni shuhguli ya msingi mno ya kuzingatiwa na mwalimu na wanafunzi.  Upimaji endelevu siyo shughuli ya mwalimu peke yake. Ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na manafunzi. Hii ni kusema kuwa, upimaji endelevu ni sehemu ya ujifunzaji wa mwanafunzi na ufundishaji wa mwalimu. Ikiwa tunahitaji kuona upimaji wenye tija, basi kila mmoja ni lazima atimize wajibu wake kwa kushirikiana. NWEA katika chapisho lao la mwaka 2016 linaloelezea mambo makuu manne ya kuzingatia ili kuleta ufanisi kwenye upimaji endelevu, wanaeleza kuwa upimaji endelevu   ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na wanafunzi wa kukusanya ushahidi wa ujifunzaji wa wanafunzi kwa lengo la kuboresha kile kinachoendelea darasani, kwa maana ya mchakato wa ujifunzaji wa wanafunzi.   Ili kufanya mchak

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?