Kutana na MAEMBE AND THE SPIRITS; wakupe CHANJO YA RUSHWA.
Ni ukweli usiopingika kuwa,Tanzania ya sasa inagubikwa na wimbi la WANAHARAKATI wa kila aina kuanzia wa kisiasa, kiuchumi na wale wa kijamii. Kimsingi katika nyanja zote za maisha ya mwananchi wa tanzania, wanaharakati wametokea kuonesha mapambano, na mara nyingi yamekuwa ni ya kujaribu kuzirekebisha taasisi au asasi husika ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zkionesha dalili ama moja kwa moja kuonesha kupindisha haki, kunyima demokrasia, kuzuia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi na matakwa ya watanzania kwa ujumla.
Maembe And The Spirits, ni miongoni mwa wanaharakati walioamua kujitosa katika msitu wenye simba wengi katika harakati za kukabiliana na tatizo sugu la RUSHWA nchini Tanzania na kwingineko duniani. Kikundi hiki, kikiongozwa na bwana Vitali Maembe, kwa kutumia nyimbo mbalimbali wanazotunga wenyewe pamoja na majadiliano ya wazi, kimeamua kwa gharama zao, kutembelea maeneo yote ya Tanzania ili kuwaelimisha watanzania mambo mbalimbali yahusuyo rushwa yakiwemo madhara, vyanzo na namna ya kuepukana na kansa hii sugu iliyomea katika damu za watu na inoyoonekana kushindwa kutibika kirahisi. Maskani yao hasa ni Bagamoyo.
Harakati yao hii wanayoiita CHANJO YA RUSHWA inayobeba ujumbe "kuiba, kutamani kuiba,kuweka mali ya wizi,kumficha mwizi, kumtamanisha mwizi ni kosa la wizi". Wanamaliza kwa kusema kuwa, "Rushwa ni Adui wa haki na maendeleo". Kwa maneno mengine, Maembe and The Spirits, wanatuambia kuwa, kula rushwa, kutamani kula rushwa,kumficha mla rushwa, kumsabibishia mtu kula rushwa ni Rushwa.
Hadi sasa wanaharakati hawa wameshatembelea katika Taasisi, wanajamii na Asasi nyingi za hapa nchini wakitoa chanjo hii ya rushwa kwa njia ya nyimbo. Haya ni mafanikio makubwa. Kwa kuwa wanaelimisha jamii kwa njia ya njimbo, pia wanapata fursa ya kuiburudisha jamii.
Kama inavyojulikana, vita dhidi ya rushwa ina maadui wengi kwa kuwa wafuasi ni wengi wasiopenda kuingiliwa. Hivyo,mbali na mafanikio waliyokwishayapata, changamoto nazo zimekuwa ni sehemu ya harakati zao. Siandiki hili kwa utashi wangu lakini mbali na kukutana na wanaharakati hawa na wakaweza kueleza miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika harakati zao za kuikabili rushwa, Bwana Vitali Maembe ameeleza hapa katika blogu yao waiitayo CHANJO YA RUSHWA miongoni mwa changamoto hizi wanazokabiliana nazo. Changamoto nyingine ni pamoja na nyimbo zao nyingine kutopewa nafasi katika baadhi ya vyombo vya habari na kushindwa kuzifikia baadhi ya taasisi kutokana na vikwazo wanavyokumbana navyo vinavyotokana na taasisi husika.
Hakika kazi wanayoifanya ni kubwa na ikizingatiwa kuwa wanajitolea. Tuwaunge mkono kwa kila hali katika harakati za kutokomeza kabisa Rushwa hapa nchini. Nimalizie kwa kusema kuwa, tabia inabadilika, rushwa ni tabia, hivyo tunaweza kubadili mitizamo yetu kwa kuikataa rushwa katika mazingira yote kama wasemavyo Maembe and The Spirits kuwa kuiba, kutamani kuiba,kuweka mali ya wizi,kumficha mwizi, kumtamanisha mwizi ni kosa la wizi.

Comments
Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!
http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html