Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"
Umewahi kuusikia au kuuona mmea uitwao Mlonge? Au kwa lugha ya kilatini "Moringa Oleivera"? Binafsi niliwahi tu kuusikia na kwa bahati nzuri hivi majuzi nilibahatika kuuona. Mmea unaoonekana pichani wenye shina kubwa ndio Mlonge wenyewe kwa mujibu wa aliyenionyesha kwani mimi sikuwahi kuuona kabla.
Mmea huu ni dawa na unaaminika kutibu magonjwa mengi yawasumbuayo binadamu pengine hata na wanyama wengine. Majani yake,matunda yake,magome yake,maua na mizizi hutumika kama dawa, kila sehemu ya mti kwa umuhimu wake.
Inasemekana matunda yake yanatumika kama mboga kwa kukatakata kama kabichi na majani yake pia hutumiwa kama mboga kwa kupika kama mchicha. Majani yake hutibu magonjwa mbalimbali na kuongeza virutubisho vya mwili.
Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment).
Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku.
Kwa mujibu wa nilikodesa,mmea huu hutibu magonjwa mengi kama shinikizo la damu,kupooza viungo au kufa ganzi,homa ya matumbo(typhoid),kuwashwa mwili,vidonda vya tumbo,malaria sugu, enia, upele n.k. Ni magonjwa mengi yaliyoorodheshwa hadi na ukimwi. Sasa sijui ilikuwa ni kutaja tu magonjwa yote yaliyopo au vipi,mimi sijui.
Dozi ya Ukimwi.
Kwa mujibu wa desa lililo na maelezo ya mmea wa mlonge, dozi ya ukimwi ni kutumia unga wa majani kijiko cha chai mara tatu kutwa kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita. Pia mgonjwa anatakiwa kutafuna mbegu tatu mara tatu kwa muda wa siku arobaini na tano sawa na wiki sita.
Unahamasishwa na kushauriwa angalao nyumbani kwako uwe na mashina kadhaa ya mmea huu kwa matumizi yako.
Comments
Kumbe tuna tabibu mbalimbali, za asili na zisizo na madhara kama ya vidonge vya makemikali na bado tunapuuza.
Nimekuwa nikiusikia huu mmea lakini sijawahi kuona na wala kujua kwa undani matumizi yake.
Shukrani saana Kaka kwa maelezo haya ya ndani juu ya mti huu.
Baraka kwako
Dawa hizi hazijapewa msisitizo wa kutosha kwa sababu pia ya ubinafsi. Wakati zamani wazee walikuwa wakiwaonyesha watoto wao miti ipi ni dawa na ipi si dawa,leo hii utaratibu huo haupo na wale wajuao miti ambayo ni dawa wamekuwa wasiri kwani kwa sasa dawa za miti shamba ni ajira za watu. Wanahofia wakisema ni majani yapi au ni mti upi unaotibu malaria basi watakuwa wamekosa soko.
Thanks
mbarikiwe