Labda B.W Botha alitumia tafsida.

P.W Botha alikuwa ni raisi wa zamani wa Afrika ya Kusini wakati nchi hii ilipokuwa inatawaliwa. Kuna wakati Raisi huyu alilihutubia baraza lake la mawaziri na nakala ya hotuba yake iliandikwa katika gazeti la Sunday times la Afrika Kusini na David G. Mailu tarehe 18 August 1985.

Botha aliongea mengi yaliyoonekana kuwakashifu waafrika. Miongoni mwa mambo aliyoyayongelea ilikuwa ni hili: "By now everyone of us has been seen it practically that Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other".
Naam, hadi sasa, nchi zote za Afrika hazitawaliwi tena na wakoloni wa kutokanchi za ng'ambo; tulishapata uhuru wa kujioongoza kama sio kujitawala. Hali halisi inaonesha tunashindwa kutumia vizuri ule uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe; uhuru ambao tuliutafuta wenyewe kwa kumwaga damu ilipobidi. Najaribu kutafakari kuhusu Afrika ya sasa. Hakuna dalili iliyowazi kweli kuwa waafrika hatuwezi kujiongoza (kidemokrasia)kama alivyosema ndugu Botha miaka kadhaa iliyopita pale aliposema: "By now everyone of us has been seen it practically that Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other"?

Kwa tafsiri ya leo, uhuru wa kujitawala umekuwa silaha mbaya sana. Tumevuka mipaka ya uhuru tulioutafuta wenyewe kwa hali na mali. Tumejitawala badala ya kujiongoza; tumerudisha matabaka ya kikoloni, watawaliwa na watawala.

Uhuru tulipewa (baada ya kuupigania). Hatua ambayo ilikuwa ya umuhimu sana.
Kwa hali ya Afrika ya sasa, naweza kusema kuwa Botha alitumia tafsida pale aliposema "give them (Africans) guns, they will kill each other". Yawezekana alimaanisha kuwa, wape waafrika uhuru, uone namna watakavyojitawala; uone namna watakavyokandamizana, uone namna watakavyoumizana na mwisho kuuana. Hawataitambua demokrasia inayowapasa: Ile ya kisiasa wala ile ya kiuchumi.

Ndiyo, tumepewa uhuru. Badala ya kujiongoza tumejitawala. Uhuru umekuwa silaha ya kukwamisha maendeleo. Uhuru umezaa wakoloni wazawa; uhuru umezaa silaha nyingi nyingine ambazo tunazitumia kuangamizana, tunazitumia kuuana kama alivyotangulia kusema ndugu Botha.

Ufisadi, rushwa, upindishaji wa sheria ziainishwazo wazi nakatiba na kugombania madaraka ya kutawala (wala si kuongoza), ni miongoni mwa silaha zilizoota mizizi baada ya uhuru (ambao mimi naona ni silaha nambari moja katika karne hii katika bara letu la Afrika) . Silaha hizi kiukweli zinatuua waafrika hususani watanzania.
Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kwa walio wengi. Tunanyanyasana, matabaka tayari yapo, tunauana wenyewe kwa wenyewe. Wazawa wachache wanatafuta kutawala (kuliko kuongoza) ili kujinufaisha wao. Wanatafuta maisha mazuri yenye kila watakalo. Wanajitahidi kurefusha maisha yao (wanazuia wao kutokufa) kwa kuua walio wengi. Tumeshuhudia migogoro ya kisiasa katika nchi nyingi za Afrika. Baadhi ni Zimbabwe, Kenya, Madagaska, Ivory Coast, Sudan, Somalia n.k. na sasa Tanzania ambapo hali ya kisiasa si ya kuridhisha. Mifano hai katika Tanzania ni mauaji yaliyotokea Zanzibar katika uchaugzi wa mwaka 2005, maualji ya watu wasio na hatia mkoani Arusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hata na yale ya Nyamongo mkoani Mara. Madhila yote haya yalikuja baada ya nguvu kubwa ya dola kutumika.
Mamia ya watu hadi sasa wapo jela pasi na hatia kwa sababu ya matumizi yasiyo stahiki ya madaraka.

Tunaodhani kuwa ni viongozi, hawaongozi bali wanatumia madaraka yao kuwachapa wanyonge kwa fimbo ya uhuru wao wa kugeuza sheria na kuzitumia kwa kadiri ya wawezavyo ili kutimiza matakwa yao. Ndio maana haishangazi kuona mahakama zetu za Kiafrika zinavyotoa maamuzi yasiyotegemewa na yasiyo ya kikatiba wala kitaaluma bali ni mashinikizo tu ya watawala fulani.
Tanzania yangu ndio hiyo inayoelekea kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wake. Ni yapi tunajivunia baada ya miaka hii hamsini? ujenzi wa barabara ama? shule za kata au? hospitali? Lakini tukumbuke kuwa wakoloni walijenga mashule na mahospitali mazuri sana, mengine hadi leo yanatumika na bado yapo imara. Labda Afrika ya Kusini isingekuwa kama ilivyo hivi sasa kama wakoloni wangeondoka miaka hamsini iliyopita.
Kwa mtazamo wangu, uhuru tuliutafuta ili tuweze kutumia uzalendo wetu kwa uhuru na kwa kiwango cha juu kabisa. Uzalendo hapa unabeba maana ya uwajibikaji wa kujituma kwa manufaa ya Taifa, jamii kwa ujumla na kwa mtu mmoja mmoja. Miaka hamsini tangu tupate uhuru.Tupo huru kutumia uzalendo wetu kuijenga nchi?
"Give Africans guns, they will kill each other", labda Botha alieleweka vibaya, ilikuwa ni tafsida tu!

Comments

Subi Nukta said…
Shukran Albert.
Nimeisambaza makala hii kwa kuwa nami umenifunza. Nimeichapisha pia kwenye blogu yangu na kurejesha credits zote kwako.
Asante kwa uelimishi.
Albert Kissima said…
Nami nakushukuru sana Dada Subi. Ninapata faraja na ninafurahi kwani mawazo yangu haya(kwa wewe kuyaweka kibarazani kwako) yatawafikia watu wengi zaidi. Shukrani sana dada.
gabriel kissima said…
Hata punda Usipombebesha mizigo basi atakifa kabla ya wakati wake.nonacho amini ,waafrika bado uwezo wetu wa kujitawala ni mdogo sana, bwana botha aikuwa sahihi akitoa kile alichokishuhudia wakati wa uongozi wake.fikra zetu zilikuwa zimejaaa hamu ya kutaka kujitawala bila ya kujiiliza kwanini wazungu waliamua kutumia nguvu kututawala?
Waafrika tunapaswa tubadilike.,....
Ni wakati sasa wa kfikiria maswala yetu ya kimaendeleo nankuacha vita.
Qalil.com said…
Asante kwa mawazo yako, ambayo ilikuwa vizuri sana samordnade.

Nadhani Botha vibaya Afrika nyeusi na kuendeshwa na wakati ambapo ilikuwa walidhani kuwa Waafrika weusi walikuwa chini kielimu savvy na hawakuweza kuelewa demokrasia.

Sisi ni kupata tu nje ya muda wakati ukabila ilitawala siku, wakati watu walitaka rais au makamu wa rais alikuja kutoka eneo fulani ya nchi (ilivyoshuhudiwa katika nchi nyumbani, Uganda).

Sasa vijana ambao kuelewa demokrasia na jinsi kazi na kuwa chini ya kuyaunganisha makabila na zaidi kwa watu katika ngazi zao kielimu (hii bila shaka, hauhusiani na kiwango cha elimu) ni mwanzo na mahitaji ya mabadiliko.

Natumaini inakuja hivi karibuni.

(I used Google translate, so if it sounds funny please forgive me)

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?