Posts

Lijue na hili

Image
Wakati mwingine wanyama(wafugwao majumbani na hata wale wa kwenye hifadhi) wanapopatwa na matatizo(mfano ugonjwa), inakuwa vigumu kutambua. Kwa kiasi kikubwa unahitajika utaalamu na uzoefu ili kuweza kugundua mapema kabla hali haijakuwa mbaya na hata kupelekea kumpoteza mnyama. Je, wafahamu dalili ya awali kabisa pale ng'ombe anapokuwa amepatwa na ugonjwa fulani? Kama unajua,ni vema,utanisadia kuboresha,na kama ulikuwa hujui,basi, ni wakati wako mzuri wa kujifunza. Kwa kawaida ng'ombe mwenye afya njema pua yake huwa na unyevunyevu wakati wote. Kwa ng'ombe ambaye ameanza au anayeshambuliwa na ugonjwa, pua yake huwa kavu kabisa. Kwa hiyo pindi uonapo pua ya ng'ombe imekuwa kavu, chukua hatua za haraka za kumuita mtaalamu kwa uchunguzi zaidi na matibabu.

Uyoga huu wa Ajabu!

Image
Dunia ina mengi ya kufurahisha na pia ya kustaajabisha kama sio kushangaza. Juzi nikiwa nyumbani nimejipumzisha chini ya mti wenye kivuli kizuri huku nikipata upepo mwanana,ghafla nilianza kuhisi harufu kama ya mzoga(mnyama aliyekufa). Harufu ile iliniwewesesha kwa kweli na ndipo iliponilazimu kuanza kufuatilia huo mzoga ambao nilijua lazima utakuwa ni wa mnyama tu. Nilifuatilia kwa makini katika eneo lile na kwa msaada wa kundi la inzi(ati wanasema inzi wana busara sana,huwa wako makini sana kutujulisha pale penye mzoga au kinyesi ili tusikanyage au kusogea karibu) niliweza kuona ulipo mzoga huo. Nilisogea karibu pamoja na harufu kali ya mzoga. Kinyume na matarajio yangu, niliuona UYOGA unaostawi vizuri ndio huo hasa uliokuwa umezingirwa na nzi pale nchani. Niliona ni vema niupige picha na kisha nikauondoa nikaenda kuutupa mbali na harufu ile ikawa imetoweka. Siku tatu baadae nikaihisi harufu ile na cha kwanza nilichofanya ni kwenda eneo lile na kukagua kama kuna uyoga wa aina ile. Kw...

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"

Image
Umewahi kuusikia au kuuona mmea uitwao Mlonge? Au kwa lugha ya kilatini "Moringa Oleivera"? Binafsi niliwahi tu kuusikia na kwa bahati nzuri hivi majuzi nilibahatika kuuona. Mmea unaoonekana pichani wenye shina kubwa ndio Mlonge wenyewe kwa mujibu wa aliyenionyesha kwani mimi sikuwahi kuuona kabla. Mmea huu ni dawa na unaaminika kutibu magonjwa mengi yawasumbuayo binadamu pengine hata na wanyama wengine. Majani yake,matunda yake,magome yake,maua na mizizi hutumika kama dawa, kila sehemu ya mti kwa umuhimu wake. Inasemekana matunda yake yanatumika kama mboga kwa kukatakata kama kabichi na majani yake pia hutumiwa kama mboga kwa kupika kama mchicha. Majani yake hutibu magonjwa mbalimbali na kuongeza virutubisho vya mwili. Maganda(magome) ya Mlonge husaidia kusafisha maji(water treatment). Mizizi hutumika kutibu watu walio na malaria sugu au watu wanaopata homa ya usiku au wanaotiririka sana jasho wakati wa homa. Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai...

Tule papai kivingine kabisa.

Papai bichi linaweza kutumika kama mboga. Twendeni jikoni pamoja. Hata wanaume tunaweza, eti haturuhusiwi kuingia jikoni! Mke akiugua au akisafiri! Twende pamoja. 1. Chukua mapapai yako mabichi yaliyokomaa ila bado kuiva. 2. Yaoshe, kisha yachonge vizuri halafu uyaoshe tena kwani yatakuwa na utomvu. 3. Yakwangue na kikwaruzio cha karoti, hapo utapata saizi ndogo ndogo kama wakati unapokwaruza karoti. Baada ya hapo, chemsha kwa muda mfupi na maji kidogo, kisha epua. 5. Kaanga kitunguu pembeni kisha weka nyanya kulingana wingi wa mboga zako, pia na karoti kama zipo, acha mchanganyiko huu uive vizuri mpaka kupata rojo ya nyanya. 6.Weka mchemsho wako wa mapapai kisha, changanya vizuri na acha mboga yako iive vizuri, pia usisahau kuweka chumvi kwa kadiri ya kipimo chako. Kwa wale wanaoweza kupata mapapai, wajaribu kupika mboga hii, ni tamu sana. Nimtakie kila mmoja atakayesoma hapa wakati mzuri na muwe na furaha kila sekunde ya maisha yenu.

WENGI HUWA HAWANA MALENGO YA KUWA WALIMU, WANALAZIMIKA.

Kulingana na tafiti niliyoifanya siku za hivi karibuni,niligundua kuwa asilimia kubwa ya waalimu wa kuanzia shule za msingi ,sekondari na hata vyuo hawakupenda kuwa walimu.Walilazimika kuwa walimu baada ya malengo yao mengine kama ya kuwa madaktari,mainjinia,wahasibu,wanasheria n.k kushindwa kutimia kutokana na kushindwa kufaulu vizuri ktk mitihani ya mwisho ya taifa kuanzia ile ya darasa la saba(kwa zamani), form four na ile ya kidato cha sita. Hata hivyo hali ya kusikitisha ni kwamba walimu wengi wanachukulia kuwa ualimu ni daraja tu na wanaamini kuwa ipo siku wataachana na kazi hiyo kwa kujiendeleza kusoma na hatimaye kufikia malengo yao ya awali.Hii hupelekea mashuleni kuwepo na walimu wasio na nia,yani bora liende,yani amekuwa mwalimu kwa sababu ilibidi.Hili liko wazi kabisa kwani waalimu wengi wameshajiendeleza na wengi wameshakuwa wahasibu,wanasheria na kadhalika. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hata jamii inaunga mkono hali hii.Mtoto anaweza kuwa na malengo ya kuwa mwalimu,lkn ...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?