Picha kutoka tovuti ya Linkedin Moja ya changamoto zinazokwamisha matumizi ya ufundishaji wa kiudadisi mashuleni ni hali ya utayari wa walimu, wakuu wa shule, viongozi wa kisiasa na wadau wengine wa elimu. Changamoto kadhaa zinatajwa kukwamisha utekelezaji wa ufundishaji na ujifunzaji huu. Baadhi zikiwemo uhaba wa nyenzo za kujifunzia na walimu kukosa maarifa ya namna ya kutumia njia za ufundishaji zainazoendana na matakwa ya mfumo huu. Hata hivyo, katikaki ya changamoto hizi, bado utekelezaji wa ufundishaji na ujifunzaji huu unawezekana. Utayari wa wadau wa elimu ndio chachu pekee ya kufanikisha hili. Palipo na utayari, changamoto kama hizi huweza kuonwa kama fursa na kuzifanyia kazi na hatimaye kufanikisha utekelezaji wa ufundishaji unaowazingatia wanafunzi. Ni heri mwalimu wa darasa la wanafunzi 50 aliye na kitabu kimoja na nia thabiti ya kut...