Posts

Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?

Sifa ya mwanafunzi anayetaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa sasa ni kuwa mbali na mambo mengine, lakini ni lazima awe na ufaulu usiopungua alama 27 daraja la IV . Kwa upande wa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada, ni lazima wawe na ufaulu wa subsidiary moja na principal pass moja kwa masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari. Vikomo hivi kwa hakika ni vya hali ya chini sana hususani kwa watu wanaotarajiwa kupewa jukumu la kufundisha. Serekali imeridhika na inalifumbia macho jambo hili kila uchao. Baada ya matokeo ya kidato cha nne, nafasi zinazotangulia kutolewa ni zile za wanafunzi watakaoendelea na masomo ya sekondari ya kidato cha tano na cha sita na wale wa chuo cha usimamizi wa maji. Wanafunzi wanaopata nafasi hizi ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu . Baada ya hapo, nafasi za ualimu hutangazwa ili waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya ngazi za juu, waombe. Mara nyingi hawa huwa ni wale wenye u...

Nimepata nafasi; ninaitumia vizuri.

Nimepata nafasi; ninaitumia vizuri Ni dhahiri shahiri kuwa watanzania wengi hatuna utamaduni wa kusoma vitabu. Kusoma vitabu ni tabia na wengi wetu hatuna tabia hii. Ila jambo la kutia moyo ni kuwa watu tuna uwezo wa kubadili tabia endapo tutakuwa na moyo wa kufanya hivyo. Mimi sikuwa na tabia ya kusoma vitabu, lakini nimejizoesha na sasa angalau kusoma vitabu pamoja na kuwa, kasi sio kubwa sana. Nimepata bahati ya kuwa mwalimu wa kuwaandaa walimu wa shule za msingi. Jukumu hili ni nyeti sana pamoja na kuwa serikali ya Tanzania haitambui umuhimu wa walimu hawa wa shule za msingi. Mazingira ya kufundishia bado ni magumu yenye kukatisha tamaa kabisa. Bila shaka, ni walimu wachache sana wenye (angalao) kuridhika na mazingira ya kazi yao ya kufundisha. Pamoja na ugumu wa kazi, lakini nimejitwika jukumu, jukumu la kuwajengea tabia na kuwakumbusha walimu watarajiwa umuhimu wa kusoma vitabu. Ninatambua nafasi waliyonayo walimu hawa wa shule za msingi katika kuk...

Shule za Msingi za Vijijini- hali bado ni tete!

Image
Ni wiki moja sasa imepita tangu nilipomaliza zoezi la kukagua maendeleo ya waalimu tarajali wanaoendelea na mafunzo yao ya kufundisha ya muda mrefu yaani "block Teaching Practice" (B.T.P). kazi ilikuwa ngumu kwani iliambatana na changamoto nyingi. shule nyingi zipo vijijini na miundo mbinu ya barabara bado ni tatizo kwa sehemu nyingi za wilaya ya Iramba. Pamoja na changamoto nyingi nilizokabiliana nazo wakati wa zoezi hili, nimepata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya vijiji vya wilaya ya Iramba na wilaya ya Singida Mjini kwa uchache. Nimepanua jiografia na kujifunza mambo mengi . Leo nitaeleza japo kwa ufupi, hali ya shule zetu za Msingi. Mazingira ya shule za msingi za Iramba bado hayaridhishi. Bado kuna idadi kubwa ya watoto wanaokaa chini. Kwa bahati mbaya madarasa ambayo wanafunzi wanakaa chini, hayana sakafu. Mfano, katika Shule ya Asanja iliyo wilaya ya Iramba, kuna madarasa ambayo hayajaezekwa, wanafunzi wanakaa chini. Pia kuna shule moja katika manispaa ya Singida,...

Kutana na MAEMBE AND THE SPIRITS; wakupe CHANJO YA RUSHWA.

Ni ukweli usiopingika kuwa,Tanzania ya sasa inagubikwa na wimbi la WANAHARAKATI wa kila aina kuanzia wa kisiasa, kiuchumi na wale wa kijamii. Kimsingi katika nyanja zote za maisha ya mwananchi wa tanzania, wanaharakati wametokea kuonesha mapambano, na mara nyingi yamekuwa ni ya kujaribu kuzirekebisha taasisi au asasi husika ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zkionesha dalili ama moja kwa moja kuonesha kupindisha haki, kunyima demokrasia, kuzuia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi na matakwa ya watanzania kwa ujumla. Maembe And The Spirits , ni miongoni mwa wanaharakati walioamua kujitosa katika msitu wenye simba wengi katika harakati za kukabiliana na tatizo sugu la RUSHWA nchini Tanzania na kwingineko duniani. Kikundi hiki, kikiongozwa na bwana Vitali Maembe, kwa kutumia nyimbo mbalimbali wanazotunga wenyewe pamoja na majadiliano ya wazi, kimeamua kwa gharama zao, kutembelea maeneo yote ya Tanzania ili kuwaelimisha watanzania mambo mbalimbali yahusuyo rushwa...

Hii ni Sayansi au Imani?

Image
Kuna mambo mengine katika hali ya kawaida, tunayatenda lakini kuyaelezea inakuwa vigumu. Tunatumia dawa na kusubiri kupona. Wengine wanatumia chakula na kusubiri wapate nguvu na kuona miili inajengeka. Maelezo ya nini kinatokea hadi haya yanafanyika, mara nyingi yanakuwa si muhimu. Picha hapo juu, inaonesha gunzi likiwa limefungwa kwenye shina na mpapai. Madhumuni ya gunzi hili ni kuzuia mpapai usiwe dume kwa maana ya kutoa maua ambayo yatatoa mapapai yasiyo ya kawaida na ambayo hayatafaa kuliwa.Nami nilishawahi kutumia njia hii miaka fulani iliyopita. Ni kweli mipapai ilikuwa inabadilika; kutoka mipapai dume na kuwa mipapai yenye kutoa mapapai mazuri yenye kufaa kula. Mapapai dume huwa yanakuwa marefu isivyo kawaida na huwa hayafai kula. Ninachojiuliza hapa ni kuwa, gunzi hili linafanyaje kazi? Labda hii ni Sayansi na pengine yapo maelezo ya kinachotokea. Au labda, hii ni imani. Kwa maana kuwa gunzi halina msaada wowote, kwamba kingine chochote kingeweza kufungwa na muhusika ak...

Labda B.W Botha alitumia tafsida.

P.W Botha alikuwa ni raisi wa zamani wa Afrika ya Kusini wakati nchi hii ilipokuwa inatawaliwa. Kuna wakati Raisi huyu alilihutubia baraza lake la mawaziri na nakala ya hotuba yake iliandikwa katika gazeti la Sunday times la Afrika Kusini na David G. Mailu tarehe 18 August 1985. Botha aliongea mengi yaliyoonekana kuwakashifu waafrika. Miongoni mwa mambo aliyoyayongelea ilikuwa ni hili: "By now everyone of us has been seen it practically that Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other". Naam, hadi sasa, nchi zote za Afrika hazitawaliwi tena na wakoloni wa kutokanchi za ng'ambo; tulishapata uhuru wa kujioongoza kama sio kujitawala. Hali halisi inaonesha tunashindwa kutumia vizuri ule uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe; uhuru ambao tuliutafuta wenyewe kwa kumwaga damu ilipobidi. Najaribu kutafakari kuhusu Afrika ya sasa. Hakuna dalili iliyowazi kweli kuwa waafrika hatuwezi kujiongoza (kidemokrasia)kama alivyosema ndugu Botha miaka kadhaa...

Soko la Magulioni-Singida Mashariki

Image
Kati ya sehemu ambazo wananchi wake wanahatarisha maisha yao, basi ni hapa katika soko hili liitwalo MAGULIONI ambalo lipo eneo maarufu liitwalo Njia panda ya Makiungu pembezoni mwa barabara ya Singida-Manyara. soko hili huwa kila siku ya Jumamosi na husheheni vitu vya kila aina kuanzia mboga mboga, nguo, kuku, miwa, vyungu, vyakula mbali mbali vikiwemo viazi vitamu vilivyopikwa na ambavvo havijapikwa, majembe n.k Kiujumla, halitofautiani na masoko mengine ambayo ulishawahi kuyaona. Mbali na upatikanaji wa vitu mbali mbali nilivyojitahidi kuvitaja, lakini pia, kila Jumamosi idadi kubwa ya watu hulitegemea sana soko hili kwa kitoweo cha nyama: kuanzia ya ng'ombe hadi ya mbuzi. Walaji wa nyama hizi kwa hakika wapo katika hatari kubwa sana kwani kulingana na uchunguzi wangu niligundua kuwa hakuna dakitari wa kuangalia uhalali wa matumizi ya nyama hizo, machinjio duni na pia sehemu za kuuzia nyama hizo ni hatari kabisa kwa afya za walaji. Picha hapa chini zinaonesha baadhi ya mabu...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?