Posts

Hii ni Sayansi au Imani?

Image
Kuna mambo mengine katika hali ya kawaida, tunayatenda lakini kuyaelezea inakuwa vigumu. Tunatumia dawa na kusubiri kupona. Wengine wanatumia chakula na kusubiri wapate nguvu na kuona miili inajengeka. Maelezo ya nini kinatokea hadi haya yanafanyika, mara nyingi yanakuwa si muhimu. Picha hapo juu, inaonesha gunzi likiwa limefungwa kwenye shina na mpapai. Madhumuni ya gunzi hili ni kuzuia mpapai usiwe dume kwa maana ya kutoa maua ambayo yatatoa mapapai yasiyo ya kawaida na ambayo hayatafaa kuliwa.Nami nilishawahi kutumia njia hii miaka fulani iliyopita. Ni kweli mipapai ilikuwa inabadilika; kutoka mipapai dume na kuwa mipapai yenye kutoa mapapai mazuri yenye kufaa kula. Mapapai dume huwa yanakuwa marefu isivyo kawaida na huwa hayafai kula. Ninachojiuliza hapa ni kuwa, gunzi hili linafanyaje kazi? Labda hii ni Sayansi na pengine yapo maelezo ya kinachotokea. Au labda, hii ni imani. Kwa maana kuwa gunzi halina msaada wowote, kwamba kingine chochote kingeweza kufungwa na muhusika ak...

Labda B.W Botha alitumia tafsida.

P.W Botha alikuwa ni raisi wa zamani wa Afrika ya Kusini wakati nchi hii ilipokuwa inatawaliwa. Kuna wakati Raisi huyu alilihutubia baraza lake la mawaziri na nakala ya hotuba yake iliandikwa katika gazeti la Sunday times la Afrika Kusini na David G. Mailu tarehe 18 August 1985. Botha aliongea mengi yaliyoonekana kuwakashifu waafrika. Miongoni mwa mambo aliyoyayongelea ilikuwa ni hili: "By now everyone of us has been seen it practically that Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other". Naam, hadi sasa, nchi zote za Afrika hazitawaliwi tena na wakoloni wa kutokanchi za ng'ambo; tulishapata uhuru wa kujioongoza kama sio kujitawala. Hali halisi inaonesha tunashindwa kutumia vizuri ule uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe; uhuru ambao tuliutafuta wenyewe kwa kumwaga damu ilipobidi. Najaribu kutafakari kuhusu Afrika ya sasa. Hakuna dalili iliyowazi kweli kuwa waafrika hatuwezi kujiongoza (kidemokrasia)kama alivyosema ndugu Botha miaka kadhaa...

Soko la Magulioni-Singida Mashariki

Image
Kati ya sehemu ambazo wananchi wake wanahatarisha maisha yao, basi ni hapa katika soko hili liitwalo MAGULIONI ambalo lipo eneo maarufu liitwalo Njia panda ya Makiungu pembezoni mwa barabara ya Singida-Manyara. soko hili huwa kila siku ya Jumamosi na husheheni vitu vya kila aina kuanzia mboga mboga, nguo, kuku, miwa, vyungu, vyakula mbali mbali vikiwemo viazi vitamu vilivyopikwa na ambavvo havijapikwa, majembe n.k Kiujumla, halitofautiani na masoko mengine ambayo ulishawahi kuyaona. Mbali na upatikanaji wa vitu mbali mbali nilivyojitahidi kuvitaja, lakini pia, kila Jumamosi idadi kubwa ya watu hulitegemea sana soko hili kwa kitoweo cha nyama: kuanzia ya ng'ombe hadi ya mbuzi. Walaji wa nyama hizi kwa hakika wapo katika hatari kubwa sana kwani kulingana na uchunguzi wangu niligundua kuwa hakuna dakitari wa kuangalia uhalali wa matumizi ya nyama hizo, machinjio duni na pia sehemu za kuuzia nyama hizo ni hatari kabisa kwa afya za walaji. Picha hapa chini zinaonesha baadhi ya mabu...

Kiswahili na Kiingereza; Twazitaka lugha hizi kwa pupa, na tunazikosa zote.

Kiswahili ni lugha kuu ya mawasiliano kwa watanzania na ndio maana inatambulika pia kama lugha ya Taifa. Kiingereza ni lugha rasmi ambayo hutumika maofisini na mashuleni, hususani shule za upili hadi vyuo vikuu. Hutumika kama lugha ya kufundishia na mawasiliano mengine. Kinyume na matarajio, sehemu ambazo kiingereza kilipaswa kutumika, maofisini na shuleni, hakitumiki ipasavyo, bali kiswahili ndicho kinachoshika hatamu. Mbali na kutoitumia lugha ya kiingereza mashuleni na kwenye ofisi, nje ya maeneo haya hali ni hiyo hiyo, watu wanatumika kiswahili kwa uhuru wao kwani ndiyo lugha pekee ituunganishayo watanzania bila kujali sana elimu aliyonayo mtu. Wapo watanzania wachache wasiokijua kiswahili vizuri kwa sababu wamekuwa wakitumia lugha za makabila yao kiasi cha kukisahau kiswahili lakini asilimia kubwa tunakizungumza vizuri. Mashuleni, walimu wanawahimiza wanafunzi wao kutumia kiingereza hata wawapo majumbani kwao kama namna ya kuijua zaidi lugha hii. Kwa mantiki hii, kiswahili kinape...

Tunazingatia matumizi ya Lazima na Hiari kwa pato letu?

Ni mda mrefu ulipita sikuonekana katika ulimwengu huu wa ku-blogu. Nilibanwa na baadhi ya majukumu, na sasa nimerudi tena na tupo pamoja. Niombe radhi kwa kutokuweka wazi juu ya adimiko langu. Naam, wakati wa adimiko, nilipata kujifunza mengi, na leo naona ni vema nigusie kidogo matumizi ya pato la mtanzania mmoja mmoja na mchango wake katika kuendeleza wimbi la umasikini au kuweza kujikwamua na umasikini. Popote pale Tanzania, mjini na vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi huonekana katika pilikapilika za hapa na pale. Wapo wafanyao kazi halali na wale wasiofanya kazi halali, lakini mwisho wa siku kila mmoja anapata ujira wake. Wapo waliojiajiri na pia walioajiriwa. Waliojiajiri, mwisho wa siku huweka chao kibindoni na wale walioajiriwa husubiri mwisho wa mwezi ndipo waweke chao kibindoni. Maisha haya humgusa yeyote yule ambaye si tegemezi katika familia au sehemu aishiyo. Huko mijini, watu huonekana kila mmoja na pilika yake ilimradi mkono uingie ki...

Mwonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kulingana na mahali mtu alipo mkoani Kilimanjaro.

Image
Muonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kwa hapa mkoani Kilimanjaro hutegemea na mahali unapouangalia mlima huu. Wilaya ya Moshi(mjini na vijijini), Rombo, na baadhi ya maeneo wilayani Hai, (Siha, Mwanga na Same sijawahi ku-view mlima Kilimanjaro hivyo sitaweza kuzungumzia mwonekano wa kilele cha Mlima kwa sasa. Pengine mwonekano hautatofautiana na wa Rombo au Moshi) kilele cha mlima huonekana kama jinsi picha inavyoonyesha hapo juu. Kwa baadhi ya maeneo kama Masama wilayani Hai na baadhi ya maeneo mkoani Arusha yanayopakana na mkoa wa Kilimanjaro. mwonekano wa kilele cha mlima ni tofauti kwani pale juu kabisa kunaonekana kuna bonde, kiasi kwamba mtu aliyeko Masama N'guni mathalani, akiambiwa achore kilele cha mlima kwa kadiri ya namna akionavyo kilele, atachora kama kinavyoonekana kwenye picha hapa chini. Nashindwa kuelewa ni kwa nini kilele ambacho ni "Iconic" ndicho ambacho huonyeshwa na hutumika zaidi kwenye picha na maonyesho mengi yahusuyo mlima huu. Kama sikupat...

Uyoga huu wa Ajabu! hatua ya awali kabisa katika uotaji wake.

Image
Hii ndio hatua ya awali kabisa ya uotaji wa Uyoga niliouelezea katika posti niliyoipa kichwa cha habari "Uyoga huu wa Ajabu". Hatua hii ya awali kama inavyoonekana, ina umbo kama la kiazi mviringo. Ni ligumu sana na ndani kuna layer mbili,moja ya rangi nyeusi na nyingine ni nyekundu. Rangi hii nyekundu bila shaka ndio inayokuja kuwa rangi ya uyoga na hii layer nyeusi ndiyo hasa inayokuja kutanda kwenye tip ya uyoga na ndio hasa iletayo harufu mbaya. Kadiri ya uyoga huu unavyozidi kukua ndivyo na umbo hili kama la kiazi mviringo linavyozidi kupungua(bila shaka sehemu kubwa ya kilichohifadhiwa ndani ni chakula kisaidiacho ukuaji wa uyoga huu). Baada ya uyoga kukua,sehemu ya nje ya umbo hili kama kiazi mviringo ambayo ni nyeupe, kama picha inavyoonyesha, huonekana kama ngozi na huwa laini ambapo ile sehemu ya ndani iliyokuwa ngumu, inabadilika na kuwa maji mazito. Ni hayo kwa leo niliyokukusanyia ndugu msomaji kuhusiana na uyoga huu mimi niuonao wa ajabu. Wapo wengi kama mimi,...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?