Uyoga huu wa Ajabu! hatua ya awali kabisa katika uotaji wake.




Hii ndio hatua ya awali kabisa ya uotaji wa Uyoga niliouelezea katika posti niliyoipa kichwa cha habari "Uyoga huu wa Ajabu". Hatua hii ya awali kama inavyoonekana, ina umbo kama la kiazi mviringo. Ni ligumu sana na ndani kuna layer mbili,moja ya rangi nyeusi na nyingine ni nyekundu. Rangi hii nyekundu bila shaka ndio inayokuja kuwa rangi ya uyoga na hii layer nyeusi ndiyo hasa inayokuja kutanda kwenye tip ya uyoga na ndio hasa iletayo harufu mbaya.



Kadiri ya uyoga huu unavyozidi kukua ndivyo na umbo hili kama la kiazi mviringo linavyozidi kupungua(bila shaka sehemu kubwa ya kilichohifadhiwa ndani ni chakula kisaidiacho ukuaji wa uyoga huu). Baada ya uyoga kukua,sehemu ya nje ya umbo hili kama kiazi mviringo ambayo ni nyeupe, kama picha inavyoonyesha, huonekana kama ngozi na huwa laini ambapo ile sehemu ya ndani iliyokuwa ngumu, inabadilika na kuwa maji mazito.



Ni hayo kwa leo niliyokukusanyia ndugu msomaji kuhusiana na uyoga huu mimi niuonao wa ajabu.



Wapo wengi kama mimi, waliokuwa wanasubiria maelezo kutoka kwa wataalamu wanaoufahamu uyoga huu. Basi, kwa niaba ya wote waliofaidika na maelezo aliyoyatoa mtaalamu kaka Bennet, nitumie muda huu kumshukuru na kumkaribisha tena na tena hapa kibarazani. Shukrani saaana kaka Bennet.

Comments

Uyoga ni chakula kizuri sana ila usipojua ni kama uyoga wa kula au unaweza kufa. Ahsante kwa shule hii.
Christian Bwaya said…
Blogu yako ni kati ya blogu zenye maarifa ya kutosha kwa wasomaji. Hongera kwa hilo mkubwa.
Albert Kissima said…
Nashukuru ndugu Christian Bwaya. Nikutakie kila la heri huko ulipo, ujifunzayo ni yetu pia, twategea mengi mazuri yatokanayo na mkutano huo wa Global voices.
Pamoja sana.

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?