Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?

Sifa ya mwanafunzi anayetaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa sasa ni kuwa mbali na mambo mengine, lakini ni lazima awe na ufaulu usiopungua alama 27 daraja la IV. Kwa upande wa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada, ni lazima wawe na ufaulu wa subsidiary moja na principal pass moja kwa masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari. Vikomo hivi kwa hakika ni vya hali ya chini sana hususani kwa watu wanaotarajiwa kupewa jukumu la kufundisha. Serekali imeridhika na inalifumbia macho jambo hili kila uchao.

Baada ya matokeo ya kidato cha nne, nafasi zinazotangulia kutolewa ni zile za wanafunzi watakaoendelea na masomo ya sekondari ya kidato cha tano na cha sita na wale wa chuo cha usimamizi wa maji. Wanafunzi wanaopata nafasi hizi ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu. Baada ya hapo, nafasi za ualimu hutangazwa ili waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya ngazi za juu, waombe. Mara nyingi hawa huwa ni wale wenye ufaulu wa kiwango cha chini na waliokosa vigezo vya kuweza kuchaguliwa kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita.
 Utaratibu huu hufanyika pia katika ngazi ya stashahada. Wale waliokosa vigezo (ambapo kigezo kikiwa ni ufaulu mdogo katika masomo ya A- Level) vya kuendelea na masomo ya elimu ya vyuo vikuu, hupewa fursra ya kuomba kujiunga na mafunzo haya ya stashahada katika vyuo mbalimbali vya ualimu hapa nchini.
Pamoja na kuwa sekta zote ni muhimu, lakini sijui ni kwa nini serikali imeamua kudharau moja kwa moja walimu kiasi cha kuendelea kubariki utaratibu huu. Imefikia mahali sasa, hata wazazi wanatoa maneno ya kejeli kwa watoto wao kwa kuwaambia kuwa wamefeli kiasi hata imeshindikana kupata nafasi ya ualimu. Hili ni tatizo kubwa, hususani kwa sekta nyeti hii ya ualimu ambayo kwa namna moja ama nyingine, inahitaji uangalizi wa kipekee kwa kuwa walimu ni miongoni mwa nyenzo muhimu inayowezesha kuwapata madaktari, manesi, waalimu, wahandisi n.k wazuri na watakaolitumikia taifa kwa ufanisi mkubwa.
Katika kikao cha kupitia rasimu ya kuandaa muongozo wa uendeshaji wa vyuo vya ualimu, nilitoa pendekezo kuwa, nafasi za kujiunga na vyuo vya ualimu kwa ngazi ya cheti ziwe zinatolewa sambamba na zile za wanaojiunga na masomo ya A level na vyuo vya ufundi na chuo cha maji .
 Hali kadhalika, nafasi za mafunzo ya ualimu ya stashahada, nayo yaende sambamba na mchakato wa kuwapata wanafunzi watakaojiunga na elimu ya juu ya vyuo vikuu. Jambo hili limeonekana haliwezekani kwa kigezo kuwa, watakaopangwa katika vyuo vya ualimu, hawataripoti katika vyuo husika, au ni wachache sana watakaojiunga na mafunzo ya ualimu. Uzoefu unathibitisha hali hii.
Sababu kubwa inayotolewa ni kuwa, ualimu hususani wa cheti na stashahada una maslahi duni sana na mazingira ya kazi ni magumu kupita kiasi. Katika mazingira haya, itakuwa vigumu sana kwa mwanafunzi mwenye vigezo vya kwenda A level aamue kwenda kupata mafunzo ya ngazi ya cheti na  kuwa mwalimu wa shule za msingi au aache kwenda kupata elimu ya chuo kikuu, aende kupata mafunzo ya stashahada ya ualimu; akawe mwalimu wa sekondari ya kata huku maslahi duni yakimuandama pamoja na mazingira duni ya kazi ambayo ni pamoja na nyumba duni za kuishi.
Mbona inakuwa rahisi sana kwa mtu kuamua kusomea uhasibu katika ngazi ya chini kabisa ya cheti? au taaluma za utabibu? Inakuwaje wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa maji wanaripoti vyuoni? Kama wangekuwa hawaripoti, basi utaratibu huu bila shaka ungeshafutwa ili kuwe na utaratibu wa kuomba kama ilivyo sekta ya ualimu na nyingie kama za unesi na upolisi.
 Ni kweli kuwa serekali hailioni jambo hili kama miongoni mwa mambo yanayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania?
 Inawezekana kuwapata waalimu wenye ufaulu mzuri wa masomo wanayofundisha endapo elimu ya ualimu utathaminiwa kwa kuboresha maslahi ya walimu kwa kiwango cha kuridhisha ikiwa ni pamoja na kutatua kero sugu kama za mazingira magumu ya kazi. Ifike mahali sasa, hata wale wanaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu nao wajiunge na mafunzo ya elimu ya ualimu.
Hili linawezekana, linawezekana pale ualimu hususani katika taasisi za umma utakapoonekana wazi kuwa una maslahi tofauti na sasa, mwalimu anavyochorwa kuwa ni mtu wa shida ambaye mara zote ni mnyonge anayedunduliza na asiye na njia mbadala ya mafanikio, yaani kupata kwake nafasi ya ualimu, imeonekana amependelewa sana kwa kuwa, kwa ufaulu wake asingeweza kupokewa popote, labda hadi akasafishe cheti.
Nitamatishe kwa kurudia kuiuliza serekali yangu, kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?

Comments

Anonymous said…
I am sure this paragraph has touched all the internet users, its really really pleasant article on building up new website.


My webpage - vestal watches for women
Anonymous said…
I'm not sure why but this site is loading very slow for me. Is anyone else having this problem or is it a issue on my end? I'll check back
later on and see if the problem still exists.


Review my website - Womens Stuhrling original Watches
Anonymous said…
Have you ever considered publishing an ebook or guest authoring on other blogs?
I have a blog centered on the same ideas you discuss and would love to have
you share some stories/information. I know my readers would appreciate your work.
If you're even remotely interested, feel free to send me an e mail.

Also visit my site ... brute force seo
Anonymous said…
Aw, this was a very nice post. Taking the time and actual effort to produce
a very good article… but what can I say… I hesitate a lot and don't manage to get anything done.

Stop by my web page; Canfriends.Com
Anonymous said…
It's remarkable in favor of me to have a web page, which is beneficial designed for my knowledge. thanks admin

Here is my blog post: womens armitron watches
Anonymous said…
We're a group of volunteers and opening a new scheme in our community. Your site provided us with valuable info to work on. You've done an impressive job and our entire community will be grateful to you.



My homepage: Relic watches

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?