Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?
Sifa ya mwanafunzi anayetaka kujiunga na mafunzo ya ualimu
ngazi ya cheti kwa sasa ni kuwa mbali na mambo mengine, lakini ni lazima awe na
ufaulu usiopungua alama 27 daraja la IV. Kwa upande wa wale
wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada, ni lazima wawe na
ufaulu wa subsidiary
moja na principal pass moja kwa masomo yanayofundishwa katika shule
za sekondari. Vikomo hivi kwa hakika ni vya hali ya chini sana hususani kwa watu wanaotarajiwa kupewa
jukumu la kufundisha. Serekali imeridhika na inalifumbia macho jambo hili kila
uchao.
Baada ya matokeo ya kidato cha nne, nafasi zinazotangulia
kutolewa ni zile za wanafunzi watakaoendelea na masomo ya sekondari ya kidato
cha tano na cha sita na wale wa chuo cha usimamizi wa maji. Wanafunzi wanaopata
nafasi hizi ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu. Baada ya hapo,
nafasi za ualimu hutangazwa ili waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya
ngazi za juu, waombe. Mara nyingi hawa huwa ni wale wenye ufaulu wa kiwango cha
chini na waliokosa vigezo vya kuweza kuchaguliwa kwa ajili ya kuendelea na
masomo ya kidato cha tano na cha sita.
Utaratibu huu
hufanyika pia katika ngazi ya stashahada. Wale waliokosa vigezo (ambapo kigezo
kikiwa ni ufaulu mdogo katika masomo ya A- Level) vya kuendelea na masomo ya
elimu ya vyuo vikuu, hupewa fursra ya kuomba kujiunga na mafunzo haya ya
stashahada katika vyuo mbalimbali vya ualimu hapa nchini.
Pamoja na kuwa sekta zote ni muhimu, lakini sijui ni kwa
nini serikali imeamua kudharau moja kwa moja walimu kiasi cha kuendelea
kubariki utaratibu huu. Imefikia mahali sasa, hata wazazi wanatoa maneno ya
kejeli kwa watoto wao kwa kuwaambia kuwa wamefeli kiasi hata imeshindikana
kupata nafasi ya ualimu. Hili ni tatizo kubwa, hususani kwa sekta nyeti hii ya
ualimu ambayo kwa namna moja ama nyingine, inahitaji uangalizi wa kipekee kwa
kuwa walimu ni miongoni mwa nyenzo muhimu inayowezesha kuwapata madaktari,
manesi, waalimu, wahandisi n.k wazuri na watakaolitumikia taifa kwa ufanisi
mkubwa.
Katika kikao cha kupitia rasimu ya kuandaa muongozo wa
uendeshaji wa vyuo vya ualimu, nilitoa pendekezo kuwa, nafasi za kujiunga na
vyuo vya ualimu kwa ngazi ya cheti ziwe zinatolewa sambamba na zile za
wanaojiunga na masomo ya A level na vyuo vya ufundi na chuo cha maji .
Hali kadhalika, nafasi
za mafunzo ya ualimu ya stashahada, nayo yaende sambamba na mchakato wa
kuwapata wanafunzi watakaojiunga na elimu ya juu ya vyuo vikuu. Jambo hili
limeonekana haliwezekani kwa kigezo kuwa, watakaopangwa katika vyuo vya ualimu,
hawataripoti katika vyuo husika, au ni wachache sana watakaojiunga na mafunzo
ya ualimu. Uzoefu unathibitisha hali hii.
Sababu kubwa inayotolewa ni kuwa, ualimu hususani wa cheti
na stashahada una maslahi duni sana
na mazingira ya kazi ni magumu kupita kiasi. Katika mazingira haya, itakuwa
vigumu sana kwa mwanafunzi mwenye vigezo vya kwenda A level aamue kwenda kupata
mafunzo ya ngazi ya cheti na kuwa
mwalimu wa shule za msingi au aache kwenda kupata elimu ya chuo kikuu, aende
kupata mafunzo ya stashahada ya ualimu; akawe mwalimu wa sekondari ya kata huku
maslahi duni yakimuandama pamoja na mazingira duni ya kazi ambayo ni pamoja na
nyumba duni za kuishi.
Mbona inakuwa rahisi sana kwa mtu kuamua kusomea uhasibu
katika ngazi ya chini kabisa ya cheti? au taaluma za utabibu? Inakuwaje
wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa maji wanaripoti vyuoni? Kama wangekuwa
hawaripoti, basi utaratibu huu bila shaka ungeshafutwa ili kuwe na utaratibu wa
kuomba kama ilivyo sekta ya ualimu na nyingie kama za unesi na upolisi.
Ni kweli kuwa
serekali hailioni jambo hili kama miongoni mwa mambo yanayochangia kushuka kwa
kiwango cha elimu Tanzania?
Inawezekana kuwapata
waalimu wenye ufaulu mzuri wa masomo wanayofundisha endapo elimu ya ualimu
utathaminiwa kwa kuboresha maslahi ya walimu kwa kiwango cha kuridhisha ikiwa
ni pamoja na kutatua kero sugu kama za mazingira magumu ya kazi. Ifike mahali
sasa, hata wale wanaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu nao wajiunge na
mafunzo ya elimu ya ualimu.
Hili linawezekana, linawezekana pale ualimu hususani katika
taasisi za umma utakapoonekana wazi kuwa una maslahi tofauti na sasa, mwalimu anavyochorwa
kuwa ni mtu wa shida ambaye mara zote ni mnyonge anayedunduliza na asiye na
njia mbadala ya mafanikio, yaani kupata kwake nafasi ya ualimu, imeonekana
amependelewa sana kwa kuwa, kwa ufaulu wake asingeweza kupokewa popote, labda
hadi akasafishe cheti.
Nitamatishe kwa kurudia kuiuliza serekali yangu, kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi
wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?
Comments
My webpage - vestal watches for women
later on and see if the problem still exists.
Review my website - Womens Stuhrling original Watches
I have a blog centered on the same ideas you discuss and would love to have
you share some stories/information. I know my readers would appreciate your work.
If you're even remotely interested, feel free to send me an e mail.
Also visit my site ... brute force seo
a very good article… but what can I say… I hesitate a lot and don't manage to get anything done.
Stop by my web page; Canfriends.Com
Here is my blog post: womens armitron watches
My homepage: Relic watches