Lijue na hili
Wakati mwingine wanyama(wafugwao majumbani na hata wale wa kwenye hifadhi) wanapopatwa na matatizo(mfano ugonjwa), inakuwa vigumu kutambua. Kwa kiasi kikubwa unahitajika utaalamu na uzoefu ili kuweza kugundua mapema kabla hali haijakuwa mbaya na hata kupelekea kumpoteza mnyama. Je, wafahamu dalili ya awali kabisa pale ng'ombe anapokuwa amepatwa na ugonjwa fulani? Kama unajua,ni vema,utanisadia kuboresha,na kama ulikuwa hujui,basi, ni wakati wako mzuri wa kujifunza. Kwa kawaida ng'ombe mwenye afya njema pua yake huwa na unyevunyevu wakati wote. Kwa ng'ombe ambaye ameanza au anayeshambuliwa na ugonjwa, pua yake huwa kavu kabisa. Kwa hiyo pindi uonapo pua ya ng'ombe imekuwa kavu, chukua hatua za haraka za kumuita mtaalamu kwa uchunguzi zaidi na matibabu.