Posts

Showing posts from November, 2017

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani? Sehemu ya Pili.

Image
Picha kutoka Mtandaoni na kuboreshwa na mwandishi wa Makala haya. Katika makala iliyotangulia, nilijadili mambo makuu mawili ambayo walimu na wanafunzi wanapaswa kuyafanya ili kuendana na mfumo wa ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi. Mamo haya mawili ni wajibu wa mwalimu na mwanafunzi na malengo ya maudhui yanayofundishwa. Makala haya yanalenga kuendelea kujadili namna nyingine tatu zinazoweza kuzingatiwa na walimu na wanafunzi ili kufanikisha utekelezaji wa mitaala inayomzingatia mwanafunzi. Kwenye makala haya, tutaaangalia wajibu wa kujifunza, nafasi ya mwalimu na mwanafunzi kuhusu masuala ya ujifunzaji na malengo ya upimaji wa mwanafunzi. Wajibu wa Kujifunza.  Wajibu wa kujifunza ni hali ya utayari wa mwanafunzi kushiriki kwenye mchakato wa ujifunzaji bila kulazimishwa ama kushurutishwa. Hali ilivyo sasa, wanafunzi wanafahamu wajibu wa mwalimu ni kuleta maarifa darasani na wajibu wa wanafunzi ni kumsikiliza mwalimu na kuandika nukuu.  Katika mfumo huu, mwa...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?