Posts

Showing posts from October, 2017

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?

Image
Kila mwanafunzi anajituma wakati wa kujifunza katika harakati za kufikia malengo yao ya ujifunzaji. Picha: Mwandishi wa makala Kama mnakumbuka, kati ya mwaka 2005 na  2007 yalitokea mabadiliko ya mitaala, hususani kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu. Kulikuwa na msemo uliovuma sana wa "muhamo wa ruwaza" au "paradigm shift" kwa kiingereza. Ruwaza ni mfumo au imani inayomuwezesha mtu kutekeleza jambo fulani kulingana na matakwa na taratibu fulani zinazofahamika. Kwenye ufundishaji, iliaminika kuwa mitaala yetu ilikuwa ya mfumo unaomuona mwalimu kama chanzo cha maarifa na mwanafunzi kama pipa linalosubiri kujazwa tu maarifa. Mitaala mipya inaaminika kuwa ya ruwaza tofauti, ndio maana mabadiliko haya yakaitwa ya kuhama kwa ruwaza. Namna mitaala ilivyoandikwa na namna ya kuitekeleza ni miongoni mwa mabadiliko haya. Kwa mfano, mabadiliko haya yalipelekea maandalio ya masomo yawe na kipengele cha upimaji kwa kila hatua ya somo. Pia, zimependekezw...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?