Walimu na Teknolojia: Zifahamu Tovuti Nzuri kwa Ajili ya Walimu

Skrinishoti ya video inayoitambulisha tovuti ya PatrickJMT

Katika makala kadhaa kwenye blogu hii, nimekuwa nikijadili kuhusu namna teknolojia zinavyoweza kutumiwa kwenye ufundishaji na ujifunzaji. Pamoja na changamoto nyingi katika mazingira ya kufundishia, bado ninaamini kuwa, matumizi ya TEHAMA kwenye ufundihsaji ni moja ya suluhisho la changamoto kadhaa za ufundishaji na ujifunzaji. Moja ya matatizo yanayoweza kutatuliwa na TEHAMA ni upungufu wa zana za kujifunzia kama vile vitabu na vyanzo vingine kama vile videos, picha, games na animations.

Kutokana na uwepo wa namna mbalimbali za watu kujifunza, nimeona nitenge muda kidogo wa kuandaa video zinazoelezea tovutinzuri kwa ajili ya walimu na wanafunzi. Ninaamini kuwa video hizi zitakuwa hamasa kwa walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanaopenda kujifunza namna mbalimbali wnavyoweza kutumia teknolojia kwenye ujifunzaji.

Ninaamini pia kuwa, hii ni hamasa kwa wale wasiopenda kusoma maandiko bali kujifunza kwa kutazama ama kufuatilia videos.

Katika makala haya, ninaitambulisha kwako Youtube channel yangu inayofahamika kwa jina la TeCh for Teachers. Chaneli hii ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kuzitambulisha tovuti nzuri kwa ajili ya walimu na wanafunzi zinazowasaidia, ama kujifunza namna ya kutumia teknolojia au kupata zana nzuri za kidigitali za kujifunzia na kufundishia.

Katika makala mbili za kwanza za video hizi, ninazitambulisha tovuti za Teacher Training Videos pamoja na PatrickJMT.

Katika tovuti ya Teacher training videos walimu wanapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali na namna wanavyoweza kuzitumia kwenye ufundishaji na ujifunzaji. Kwa ufahamu zaidi kuhusu tovuti hii, unaweza kufuatili video hii hapa kwa ajili ya kujifunza zaidi.

Katika tovuti ya PatrickJMT, wanafunzi na walimu wanapata fursa ya kujifunza Hisabati kwa kufuatilia video mbalimbali. Mada mbalimbali kama vile Calculus, Algebra, Arthmetic na nyingine nyingi zimejadiliwa sambamba na mifano.Kwa ufahamu zaidi kuhusu tovuti hii, unaweza kufuatili video hii hapa kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Kama utapendezwa na video hizi, usisahau kujisajili kwa kubonyeza "subscribe" ili usipitwe na video zinazozitambulisha tovuti nzuri kwa ajili ya ujifunzaji na ufundishaji.




Comments

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?