Walimu na Teknolojia: Zifahamu Tovuti Nzuri kwa Ajili ya Walimu
Skrinishoti ya video inayoitambulisha tovuti ya PatrickJMT Katika makala kadhaa kwenye blogu hii, nimekuwa nikijadili kuhusu namna teknolojia zinavyoweza kutumiwa kwenye ufundishaji na ujifunzaji. Pamoja na changamoto nyingi katika mazingira ya kufundishia, bado ninaamini kuwa, matumizi ya TEHAMA kwenye ufundihsaji ni moja ya suluhisho la changamoto kadhaa za ufundishaji na ujifunzaji. Moja ya matatizo yanayoweza kutatuliwa na TEHAMA ni upungufu wa zana za kujifunzia kama vile vitabu na vyanzo vingine kama vile videos, picha, games na animations. Kutokana na uwepo wa namna mbalimbali za watu kujifunza, nimeona nitenge muda kidogo wa kuandaa video zinazoelezea tovutinzuri kwa ajili ya walimu na wanafunzi. Ninaamini kuwa video hizi zitakuwa hamasa kwa walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanaopenda kujifunza namna mbalimbali wnavyoweza kutumia teknolojia kwenye ujifunzaji. Ninaamini pia kuwa, hii ni hamasa kwa wale wasiopenda kusoma maandiko bali kujifunza kwa kutazama am...