Unapenda Kutumia Vitumizi vya Android kwenye Kompyuta Yako? Mfumo Endeshi wa Remix ni Jibu Lako.
Skrinishoti kutoka Tovuti ya RemixOS Hakuna shaka kuwa ili uifaidi simu yako vizuri, inapendeza sana ikiwa utaweza kuweka vitumizi (applications) unavyovipenda. Ni muhimu kutambua kuwa, aina na wingi wa vitumizi vizuri unavyoweza kuvitumia hutegemea na aina ya Mfumo Endeshi (Operating System) wa simu au kifaa chako. Hii ina maana kuwa, unaponunua simu, ni vyema ukafahamu ni aina gani ya Mfumo Endeshi ungependa kuutumia na ikiwa utakuwezesha kutumia vitumizi unavyovipenda. Kwa sasa, moja ya Mfumo Endeshi pendwa kabisa wa simu ni Android. Ni dhahiri kuwa, Mfumo Endeshi huu una mkusanyiko wa vitumizi vizuri sana kwa simu. Haishangazi kuona kitumizi fulani kinapatikana kwenye Android lakini hakiwezi kutum...