Shairi: Kilio cha Albino
Picha kutoka Yahoo news Kisa ni mbovu imani, Ndugu zetu mwawaua, [ Amir Kulanteni] Mwamuabudu shetani, Mmezitupa sheria, Twapita tu duniani, Kifo chaja kwenu pia, Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? Wenye dhima mwafanyani? Uhai kutulindia, Wananchi mashakani, Nyie kiguu na njia, Mara mpo marekani, Sisi huku tunalia, Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? Mwaiba mabilioni, Mwashindwa kututetea, Ni kama watu usoni, Moyoni mwatumendea, Ni kama tu hayawani, Imani zimepotea, Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? Vitendo vyangoja nini?, Matamko tu mwatoa, Ndugu zetu kaburini, Hamuioni kadhia, Matendo ya kishetani, Nyie mwayakaushia, Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? Twendeni makanisani, Tuombe huku twalia, Twendeni misikitini, Tuzisome kali dua, Mungu na awalaani, Motoni aje watia, Kilio cha Albino, Hivi kweli tunajali? A...