Ni Kukua kwa Kiswahili, Kuporomoka au ni Mwanzo wa lugha Nyingine?
Pamoja na kuwa Kiingereza ndio lugha rasmi ya kufundishia katika shule za sekondari na vyuo vikuu, ni muda mrefu sasa kumekuwa na mijadala ya lugha ipi kati ya hizi mbili ni muafaka katika kufundishia. Mijadala hii inakuja kufuatia kuendelea kudorora kwa ubora wa elimu nchini Tanzania. Kuhusiana na hili, tafiti nyingi zimeshafanyika. Lengo si kujadili tafiti hizi, wala ni lugha ipi ni muafaka katika kufundishia wanafunzi nchini Tanzania. Hii inaonesha kuwa Tanzania tuna utata katika matumizi ya Kiswahili na Kiingereza. Utata unaohitaji suluhisho. Watanzania tulio wengi tumekuwa na tabia ya kuchanganya lugha ya Kiswahili na kiingereza katika kuongea. Bahati mbaya sana wengi wa watumiaji wa mseto huu ni wasomi au waswahili waliopata bahati ya kujua maneno machache ya kiingerezaa au ni waongeaji wazuri wa Kiingereza. Kwa mtazamo wangu, hili ni tatizo letu watanzania. Tena ni tatizo la msingi kabisa. Kiswahili ni moja ya utambulisho wetu watanzania. Huu ni utambaduni ...