Singida: Wananchi Wakubali Malazi Bora katika Bora Mazingira-Sehemu ya Kwanza





Nyumba ya asili ya wakazi wa Mkoani Singida, maarufu kwa jina la "Tembe"

Bila shaka umewahi kuzisikia ama kuziona nyumba zinazoezekwa kwa kutumia udongo badala ya bati almaarufu kama “tembe”. Nyumba hizi zinapatikana kwa wingi katika mkoa wa Singida na hata katika mikoa mingine kama vile Dodoma. Nyumba hizi za tembe ni za kiasili kwa mkoa huu wa Singida. Hadi sasa nyumba hizi bado zinatumika kwa kiasi kikubwa tu kama nyumba kwa ajili ya malazi ya wakazi wa mkoa huu.

Miaka ya hivi karibuni, wakazi wa mkoani Singida wameanza kujenga nyumba zilizo bora zaidi. Wakazi hawa wamejikita katika ujenzi wa nyumba za kuishi kwa kutumia matofali ya kuchoma. Taratibu wanaachana na ujenzi wa nyumba za tembe pamoja na kuwa, kwa kiasi fulani, katika ujenzi wa makazi haya bora, wamekuwa wakihamishia namna fulani ya ujenzi unaoshabihiana na ule wa nyumba za tembe. Mfano, nyumba za tembe huwa zinakuwa na vidirisha vidogo vidogo. Zipo pia baadhi ya nyumba bora zilizojengwa kwa matofali ya kuchoma huku zikiwa na madirisha madogo sana kiasi cha kutoruhu hewa ya kutosha kuingia na kutoka ndani ya nyumba.

     Picha za nyumba za kisasa zinazojengwa kwa matofali ya kuchoma

Nia ya makala hii ni kuelezea muamko wa ujenzi  wa makazi bora kwa wananchi wa Singida na faida na hasara ya kushamiri kwa ujenzi  wa makazi haya bora. Ninaweza kusema, takribani asilimia 95 ya nyumba bora zinazojengwa mkoani Singida, hutumia  matofali ya kuchoma. Lakini hebu tujiulize, matofali haya huandaliwa vipi?

Hili ni tanuru la matofali yaliyokwisha chomwa lakini baadhi ya matofali hayakuiva vyema, hivyo yale ambayo hayakuiva, yamepangwa tena kwa ajili ya kuchomwa. Pembeni ni lundo la kuni mbichi kwa ajili ya kuchomea matofali.

Uandaaji wa matofali haya unahitaji udongo, maji na kuni za kuyachomea matofali yaliyoandaliwa. Picha hapo juu inaonesha matofali yaliyopangwa kwa ustadi mkubwa ili yachomwe. Pembeni ni lundo la kuni zitakazotumika kwa ajili ya kuchomea matofali. Matofali hupangwa kwa utaalamu sana ili kutengeneza mpangilio wa matofali  ujulikanao kama “tanuru”. Tanuru ni mjumuiko wa matofali yanayochomwa pamoja na kuni/ magogo mabichi ya miti. Tanuru hufunikwa vizuri kwa tope ili hewa isiingie ndani wakati kuni/ magogo mabichi yakiwaka na hatimaye kuyachoma matofali.

                   Tanuru la matofali yaliyokwisha chomwa

Udongo unaotumika kuandalia matofali ni wa tabaka la juu. Haimlazimu mtu kuchimba kwa kina kirefu ili kupata udongo mzuri kwa ajili ya kuandalia matofali. Ndio maana haitashangaa kuona mtu ameandaa matofali pembeni tu ya nyumba yake ya tembe. Kwa hakika, udongo huu wa juu ndio wenye rutuba na ndio unaotegemewa kwa ajili ya mazao ya chakula kwa wakazi hawa. Lakini kwa upande mwingine, wanajikomboa kwa kutengeneza nyumba bora zaidi kwa ajili ya kuishi.
Uandaaji wa matofali umeacha maeneo mengi yakiwa na mashimo na bila kuwa na njia muafaka za kufukia mashimo hayo. Tabaka la juu la udongo ndilo hasa linalotumiwa katika ujenzi wa matofali. Mimomonyoko ya udongo haiepukiki hususani wakati wa mvua. Mabo haya wananchi hawayatilii maanani, wao wamelenga kujenga makazi bora ya kuishi.
Tumeona kuwa, uandaaji wa matofali unahitaji kuni kwa ajili ya kuyachoma. Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, kuni au magogo ya kuchomea matofali yanatoka wapi. Mazingira yanasalimika kweli? Misitu isababishayo uwepo wa mvua inasalimika kweli? Nitaiendeleza makala hii wakati ujao.

Wakati wananchi wakiiacha ardhi yao katika hali ya mshimo na kukaribisha mmomonyoko wa udongo, ikumbukwe kuwa, Singida ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na ukame uliopitiliza.




Comments

Anonymous said…
"Whoever believes in Jesus will have everlasting life." Kinda. Theoretically. What they will experience is the perpetual life cycle of birth-aging-death on Earth-like planets. It ensures a second chance for those who fell for the god's deception and are too stupid to pull out of it in a timely manner, for only the true believers (Flanders) will survive come transplant/colonization.
I believe these people are the original residents of a planet (Earth=Africans). Other regions are populated with groups whom are transplaned as the gods deem fit (Native Americans=next Asians, Ashkenaz Jews=next Europeans).
Believing this deviate pimp Jew is god comes at a price, reflected in blacks strengths/weaknesses.
Ironically, due to the god's positioning the Antients ensured these people would not receive two second chances:::Christianity is an Italian religion, responsible for black misery ranging from slavery to the crack epidemic and Italian-style gang membership.
Incidentally, although I ridicule the idea Jesus is god I am slated for this group on the next planet Earth for my unwillingness to bow to absolute power and, like the black man, will be reincarnated less capable compared to my fellow man. And that's why the gods created this reputation among the black man. As far as why Jewish men are like faggotty...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?