Tanzania Iliyobarikiwa Isiyo ya Wabarikiwa

Picha ya Muonekano wa Kaldera ya Ngorongoro

Tanzania inajulikana kuwa na rasilimali nyingi sana ambazo kama zingetumika vizuri, basi watanzania tungekuwa katika hali nafuu sana ya maisha kuliko hivi sasa. sitamani kuwakumbusha utajiri ambao nchi ya Tanzania ilionao kwani umeshakuwa ni wimbo ambao kwa sasa pengine hakuna tena anayetaka kuusikiliza kabisa. Kama nilivyotangulia kusema katika bandiko lililopita, nilipata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya mkoa wa Singida, hususani wilaya ya Iramba. nilisema pia, kuna mengi niliyojifunza kwa kusimuliwa na kwa kujionea mwenyewe. leo nitawajuza kuhusu mgodi mpya wa dhahabu nilioushuhudia katika ukanda wa bonde la ufa la sekenke katika eneo liitwalo Mgongo.

Mgodi wa Mgongo uko wilaya ya Iramba-sekenke, kama mita mia mbili kutoka ilipo shule ya msingi  Mgongo; shule ambayo ndiyo niliyofikia kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya waalimu walio katika mafunzo ya muda mrefu ya kufundisha. Nilifika hapo tarehe 07/03/2012 na nilipewa taarifa kuwa kuna mgodi wa dhahabu karibu kabisa na shule hiyo na kwamba wenyeji walishaanza kuyafaidi mamilioni kutokana na mgodi huo. niliambiwa kuwa mgodi huu wa Mgongo uligunduliwa wiki mbili toka siku niliyofika hapo shuleni Mgongo.

Nilipata fursa ya kuutembelea mgodi huu na nilishuhudia watu (wenyeji) wakiendelea na shughuli za uchimbaji madini. baadhi ya mashino yalikuwa tayari yameenda sana chini na wenye mashimo tayari walikuwa wameshapata madini na kuyauza na kujipatia fedha. Mashimo mengine ndio yalikuwa yanaanzwa na mengine bado walikuwa hawajakuta mwamba mgumu wenye madini. Hii ilitosha kunijulisha kuwa mgodi huu haukuwa wa siku nyingi. mgodi huu wa Mgongo bado ni wa wenyeji lakini siku si nyingi watakuja watu wa kila aina kutoka pande zote za Tanzania na hatimaye wawekezaji wa kigeni.

Mgodi huu umeongeza idadi ya migodi katika ukanda huu wa sekenke. Migodi mingine iliyoko Singida ni kama Mgodi wa dhahabu wa Misigiri ulioko Iramba na ule wa Londoni ulioko Manyoni . Bila shaka bado tuna hazina kubwa ya madini mbalimbali yakiwemo haya ya dhahabu na mengine mengi kama ya shaba, almasi, Tanzanite na kadhalika. Hatujibidishi kuvumbua hazina nyingine ya rasimali asilia tulizo nazo bali hutokea kwa bahati tu. Hakuna makusudi kamili ya kusubiri muda muafaka wa kuchimba madini kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.

Nchi ya Tanzania ina kila sababu ya kutokutegemea misaada kutoka nchi nyingine, hili linawezekana kabisa hasa ukizingatia rasilimali tulizonazo. Kinachotuangusha ni sisi rasilimali watu, japokuwa sio wote lakini wanaotuangusha ni watu. Madini yangekuwa na uwezo wa kusema, basi yangeshasema, hifadhi zingekuwa na uwezo wa kusema, zingeshasema namna ambavyo nyumba yao ya Tanzania isivyotendewa haki. Mwalimu Nyerere alizitanabaisha nguzo muhimu za kuweza kupata maendeleo, miongoni mwa nguzo hizo ni uongozi bora. Tunaweza kutoa lawama kwa viongozi wetu lakini tukiangalia kwa undani zaidi, tutakuta tatizo lipo kwetu sisi wa-Tanzania. Ndio, tatizo lipo kwetu sisi. Ndio maana sichelei kusema kuwa, nchi yangu ya Tanzania imebarikiwa lakini hakuna wabarikiwa.

Nimegusia tu baadhi ya rasilimali za madini zilizopo mkoani Singida. Lakini Tanzania tuna rasilimali za kila aina na zilizo za kipekee kabisa barani Afrika na duniani kote. Milima ya kuvutia, mabonde, hifadhi asilia za wanyama kama Kaldera ya Ngorongoro, bahari, bandari na hata tamaduni za makabila mbalimbali zenye kuvutia. "Rasilimali zetu hatuzitumii ipasavyo", huu ni wimbo usiochuja miongoni mwetu watanzania. Bado hatujaridhika na huduma za afya, elimu, usafiri na sekta nyingize zote pamoja na kuwa na neema ya rasilimali nyingi tulizo nazo.

Watanzania tunajipangaje kuepuka kuendelea kuuimba wimbo huu wa "Rasilimali zetu hatuzitumii ipasavyo"Ni dhahiri kuwa, bado hatujapa usimamizi mzuri wa rasilimali tulizonazo. Mfumo wa uongozi bado haujaweza kuzisimamia rasilimali hizi kwa manufaa ya taifa. Mwalimu Nyerere alituambia kuwa Uongozi usio bora ni chanzo cha kukwamisha maendeleo. Tanzania bado hatujafika tunapopataka. Uongozi uliopo ni kwa ridhaa yetu.  Tunapoulalamikia, ni dhahiri kuwa tunajilalamikia wenyewe na tena kujikosoa wenyewe. 

Hebu watanzania tujipange, tutambue tunataka nini, tuweke mikakati ya dhati. Na kwa kukumbusha tu ni kuwa, tuwe makini sana tunapopata fursa ya kuwachagua viongozi mbalimbali wa Taifa letu kwani usimamizi mzuri wa rasilimali zetu ni chanzo cha ustawi wetu. Ikibidi tubadili mfumo wa uongozi, ni jukumu letu watanzania tunapoelekea mwaka 2015, mwaka wa fursa nyingine ya kuamua mustakabali wa Tanzania yetu Ililobarikiwa Isiyo ya Wabarikiwa.


Comments

nakuunga mkono asilimia 100%
Anonymous said…
7:45p
"You'll pay first." Arsenic complications arising from rice consumption. "(Because as evil they attackk good.)" It's YOUR doing, conducting your motherfuckking theater. Much like everything else here I have to pay for it.
I pay first because I'm so good and Asians are the most evil on Planet Earth, as evident by intelligent design's clues.
"Buy rice grown in California." and skip the Asian shit. "We got some worked up." Some Italians too:::Clone host fake trillionaires. The Antients are the depraved monsters destroying life on Planet Earth. Using this legwork they will not accept culpability and incurr any blame.
"We're not changing." I'm not askking you to. After a lifetime of sacrifice I do expect a job I can live with, a job that accomodates the problems you created, likke social and clothing. You had the opportunity to position corporate compassion and you chose this way instead.

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?