TUZO ZA WALIMU BORA TANZANIA 2012-2013
Kwa mujibu wa kamati ya uratibu wa tuzo hizi inayoongozwa na ndugu Clemence A. Kambengwa, tuzo hizi zinaandaliwa na asasi iitwayo EDUCATION AND EXPEDITION AGENCY ASSOCIATION.
Taarifa ya Kamati ya Uratibu ya tuzo hizi inaendelea kueleza kuwa, tuzo hizi za kihistoria hapa nchini zitashirikisha walimu wa shule za msingi na shule za Sekondari kutoka nchi nzima. Mchakato unaendelea, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa taratibu zote za maadalizi. Taarifa rasmi kuhusu zawadi zitatolewa wakati wa uzinduzi ila matarajio ya zawadi kwa washindi zitakuwa ni zawadi za aina yake ambazo hazijawahi kutolewa hapa nchini.
Uzinduzi rasmi wa Tuzo hizi unatarajiwa kufanyika Nov 20/2012 na kilele chake itakuwa ni Tarehe 25/NOV 2013.
Taarifa zaidi zitazidi kutolewa kuhusiana na tuzo hizi.
Taarifa hii (kama nilivyotangulia kutaja) ni kwa mujibu wa Kamati ya Uratibu ya tuzo hizi za kihistoria za Walimu inayoongozwa na ndugu Clemence A. Kambengwa (Event Director, info@eeaa.or.tz/0762000505)
Comments