Wizara ya Elimu: kwa nini inaridhika kudahili wanafunzi wenye ufaulu wa kiwango cha chini katika vyuo vya ualimu?
Sifa ya mwanafunzi anayetaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa sasa ni kuwa mbali na mambo mengine, lakini ni lazima awe na ufaulu usiopungua alama 27 daraja la IV . Kwa upande wa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada, ni lazima wawe na ufaulu wa subsidiary moja na principal pass moja kwa masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari. Vikomo hivi kwa hakika ni vya hali ya chini sana hususani kwa watu wanaotarajiwa kupewa jukumu la kufundisha. Serekali imeridhika na inalifumbia macho jambo hili kila uchao. Baada ya matokeo ya kidato cha nne, nafasi zinazotangulia kutolewa ni zile za wanafunzi watakaoendelea na masomo ya sekondari ya kidato cha tano na cha sita na wale wa chuo cha usimamizi wa maji. Wanafunzi wanaopata nafasi hizi ni wale wenye ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu . Baada ya hapo, nafasi za ualimu hutangazwa ili waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya ngazi za juu, waombe. Mara nyingi hawa huwa ni wale wenye u...