Shule za Msingi za Vijijini- hali bado ni tete!

Ni wiki moja sasa imepita tangu nilipomaliza zoezi la kukagua maendeleo ya waalimu tarajali wanaoendelea na mafunzo yao ya kufundisha ya muda mrefu yaani "block Teaching Practice" (B.T.P). kazi ilikuwa ngumu kwani iliambatana na changamoto nyingi. shule nyingi zipo vijijini na miundo mbinu ya barabara bado ni tatizo kwa sehemu nyingi za wilaya ya Iramba. Pamoja na changamoto nyingi nilizokabiliana nazo wakati wa zoezi hili, nimepata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya vijiji vya wilaya ya Iramba na wilaya ya Singida Mjini kwa uchache. Nimepanua jiografia na kujifunza mambo mengi . Leo nitaeleza japo kwa ufupi, hali ya shule zetu za Msingi.

Mazingira ya shule za msingi za Iramba bado hayaridhishi. Bado kuna idadi kubwa ya watoto wanaokaa chini. Kwa bahati mbaya madarasa ambayo wanafunzi wanakaa chini, hayana sakafu. Mfano, katika Shule ya Asanja iliyo wilaya ya Iramba, kuna madarasa ambayo hayajaezekwa, wanafunzi wanakaa chini. Pia kuna shule moja katika manispaa ya Singida, tulikuta watoto wamekaa chini darasani. Mazingira haya ni hatarishi kwa masomo na kwa afya zao. Picha hapa chini, ni ya wanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi Ipuli iliyo katika wilaya ya Iramba. Idadi kubwa ya wanafunzi wanakaa chini. Hili ni darasa moja, darasa la tatu hali kadhalika, hata na madarasa mengine, hali ingekuwa hivi ni vile tu walilazimishwa kubanana kwnye madawati machache kwa ajili ya ukaguzi.



Picha hapa chini ni ya wanafunzi wa darasa la tatu, shule ya msingi Ipuli. wanaonekana wengine wakiwa mamekaa kwnye madawati kwa kubanana na wengine wakiwa wamekalia masalia ya madawati. Darasa halina sakafu, ni vumbi linalotisha. Angalao. hawa wamejinasua kenye kuliogelea vumbi hili kwa kukalia masalia ya madawati japokuwa bado sikubaliani na mazingira ya kusomea ya aina hii.
Kwa upande mwingine, wazazi/ walezi nao wanaonekana kutokutimiza wajibu wao vizuri. wanafunzi wanakuja  shuleni wakiwa katika hali isiyoridhisha. Asilimia kubwa ya wanafunzi si wanadhifu kwa maana kuwa mbali na sare zao kuwa chafu pia ziko katika hali ya kuchakaa sana. bila shaka hali hii inachangiwa na umasikini na wazazi/ walezi kutokuwa na muamko stahiki wa elimu. Baadhi ya shule nilielezwa kuwa wazazi/ walezi badala ya kuwa chachu ya maendeleo ya watoto wao, wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa kutokutoa ushirikiano stahiki kwa uongozi wa shule na kwa walimu kwa ujumla.

Nimesikia fedha za rada zilizorejeshwa, zimeelekezwa kwenye elimu na hususani elimu ya msingi haswa haswa katika kuboresha mazingira ya kusomea. Bila shaka hali ya shule za vijiji vya Iramba inawakilisha hali ya shule nyingine nyingi katika vijiji vyetu vya Tanzania. Naikumbusha serikali kuzitazama kwa jicho la huruma shule hizi. Mamilioni hayo ya Rada yaboreshe shule hizi ili elimu ya msingi iliyokusudiwa kwa watoto hawa iwafikie kwa kiwango cha kuridhisha. Serikali ikumbuke kuwa uboreshaji ni pamoja na kuwakumbuka wale waliopewa jukumu la kusimamia mafunzo hayo ya elimu ya msingi. Mazingira ya ufundishaji nayo yaboreshwe ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa vitendea kazi, malazi bora kwa walimu na ulipaji wa mishahara na madai yao mengine kwa wakati.

Comments

chib said…
Hivi na ile michango ya madawati kwa kila mwananfunzi anayeanzan shule huwa ianafanyia nini, au wanafunzi wakimaliza darasa la saba basi yanakuwa yamevunjika au wanaondoka nayo? Mbona kila mwaka madawati yakiongezeka ni yale yaliyotolewa na wasamaria wema au kwenye kampeni za kisiasa
Albert Kissima said…
Hapo sasa ndugu Chib, hapa wazazi wana la kujibu. Ila kama nilivyotangulia kusema, mwamko wa elimu kwa wazazi/walezi vijijini bado ni mdogo hivyo hawaoni sana umuhimu wa hata kuchangia madawati. Bila shaka hata na waalimu watakuwa kwa namna moja ama nyingine wanahusika.

Bahati nzuri (ama mbaya), shule nyingi za vijijini ziko chini ya mpango wa US AID unaotoa msaada wa chakula ktk shule za msingi. Shule niliyopiga picha hizi, msaada huu haujawafikia bado. Wazazi waliambiwa wachange hela ya chakula cha watoto wao, wakagoma. Hali imepelekea watoto kurudi nyumbani kwenda kula. Wale wanaotokea mbali sana na shule wanalazimika kuvumilia hadi watakaporudi nyumbani jioni. Kibaya zaidi ni pale mtoto huyu anaposhinda siku nzima bila kula, halafu si ajabu hata chai (angalau ya mkono mmoja) hakupata na cha kusikitisha mlo mmoja wa usiku nao unakuwa ni wa kubahatisha usio kamili.
Tammy Davis said…
Hapo sasa ndugu Chib, hapa wazazi wana la kujibu. Ila kama nilivyotangulia kusema, mwamko wa elimu kwa wazazi/walezi vijijini bado ni mdogo hivyo hawaoni sana umuhimu wa hata kuchangia madawati. Bila shaka hata na waalimu watakuwa kwa namna moja ama nyingine wanahusika. Bahati nzuri (ama mbaya), shule nyingi za vijijini ziko chini ya mpango wa US AID unaotoa msaada wa chakula ktk shule za msingi. Shule niliyopiga picha hizi, msaada huu haujawafikia bado. Wazazi waliambiwa wachange hela ya chakula cha watoto wao, wakagoma. Hali imepelekea watoto kurudi nyumbani kwenda kula. Wale wanaotokea mbali sana na shule wanalazimika kuvumilia hadi watakaporudi nyumbani jioni. Kibaya zaidi ni pale mtoto huyu anaposhinda siku nzima bila kula, halafu si ajabu hata chai (angalau ya mkono mmoja) hakupata na cha kusikitisha mlo mmoja wa usiku nao unakuwa ni wa kubahatisha usio kamili.

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?