Kiswahili na Kiingereza; Twazitaka lugha hizi kwa pupa, na tunazikosa zote.
Kiswahili ni lugha kuu ya mawasiliano kwa watanzania na ndio maana inatambulika pia kama lugha ya Taifa. Kiingereza ni lugha rasmi ambayo hutumika maofisini na mashuleni, hususani shule za upili hadi vyuo vikuu. Hutumika kama lugha ya kufundishia na mawasiliano mengine. Kinyume na matarajio, sehemu ambazo kiingereza kilipaswa kutumika, maofisini na shuleni, hakitumiki ipasavyo, bali kiswahili ndicho kinachoshika hatamu. Mbali na kutoitumia lugha ya kiingereza mashuleni na kwenye ofisi, nje ya maeneo haya hali ni hiyo hiyo, watu wanatumika kiswahili kwa uhuru wao kwani ndiyo lugha pekee ituunganishayo watanzania bila kujali sana elimu aliyonayo mtu. Wapo watanzania wachache wasiokijua kiswahili vizuri kwa sababu wamekuwa wakitumia lugha za makabila yao kiasi cha kukisahau kiswahili lakini asilimia kubwa tunakizungumza vizuri. Mashuleni, walimu wanawahimiza wanafunzi wao kutumia kiingereza hata wawapo majumbani kwao kama namna ya kuijua zaidi lugha hii. Kwa mantiki hii, kiswahili kinape...