Mwonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kulingana na mahali mtu alipo mkoani Kilimanjaro.
Muonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kwa hapa mkoani Kilimanjaro hutegemea na mahali unapouangalia mlima huu. Wilaya ya Moshi(mjini na vijijini), Rombo, na baadhi ya maeneo wilayani Hai, (Siha, Mwanga na Same sijawahi ku-view mlima Kilimanjaro hivyo sitaweza kuzungumzia mwonekano wa kilele cha Mlima kwa sasa. Pengine mwonekano hautatofautiana na wa Rombo au Moshi) kilele cha mlima huonekana kama jinsi picha inavyoonyesha hapo juu. Kwa baadhi ya maeneo kama Masama wilayani Hai na baadhi ya maeneo mkoani Arusha yanayopakana na mkoa wa Kilimanjaro. mwonekano wa kilele cha mlima ni tofauti kwani pale juu kabisa kunaonekana kuna bonde, kiasi kwamba mtu aliyeko Masama N'guni mathalani, akiambiwa achore kilele cha mlima kwa kadiri ya namna akionavyo kilele, atachora kama kinavyoonekana kwenye picha hapa chini. Nashindwa kuelewa ni kwa nini kilele ambacho ni "Iconic" ndicho ambacho huonyeshwa na hutumika zaidi kwenye picha na maonyesho mengi yahusuyo mlima huu. Kama sikupat...