Tule papai kivingine kabisa.
Papai bichi linaweza kutumika kama mboga. Twendeni jikoni pamoja. Hata wanaume tunaweza, eti haturuhusiwi kuingia jikoni! Mke akiugua au akisafiri! Twende pamoja. 1. Chukua mapapai yako mabichi yaliyokomaa ila bado kuiva. 2. Yaoshe, kisha yachonge vizuri halafu uyaoshe tena kwani yatakuwa na utomvu. 3. Yakwangue na kikwaruzio cha karoti, hapo utapata saizi ndogo ndogo kama wakati unapokwaruza karoti. Baada ya hapo, chemsha kwa muda mfupi na maji kidogo, kisha epua. 5. Kaanga kitunguu pembeni kisha weka nyanya kulingana wingi wa mboga zako, pia na karoti kama zipo, acha mchanganyiko huu uive vizuri mpaka kupata rojo ya nyanya. 6.Weka mchemsho wako wa mapapai kisha, changanya vizuri na acha mboga yako iive vizuri, pia usisahau kuweka chumvi kwa kadiri ya kipimo chako. Kwa wale wanaoweza kupata mapapai, wajaribu kupika mboga hii, ni tamu sana. Nimtakie kila mmoja atakayesoma hapa wakati mzuri na muwe na furaha kila sekunde ya maisha yenu.