WENGI HUWA HAWANA MALENGO YA KUWA WALIMU, WANALAZIMIKA.

Kulingana na tafiti niliyoifanya siku za hivi karibuni,niligundua kuwa asilimia kubwa ya waalimu wa kuanzia shule za msingi ,sekondari na hata vyuo hawakupenda kuwa walimu.Walilazimika kuwa walimu baada ya malengo yao mengine kama ya kuwa madaktari,mainjinia,wahasibu,wanasheria n.k kushindwa kutimia kutokana na kushindwa kufaulu vizuri ktk mitihani ya mwisho ya taifa kuanzia ile ya darasa la saba(kwa zamani), form four na ile ya kidato cha sita.

Hata hivyo hali ya kusikitisha ni kwamba walimu wengi wanachukulia kuwa ualimu ni daraja tu na wanaamini kuwa ipo siku wataachana na kazi hiyo kwa kujiendeleza kusoma na hatimaye kufikia malengo yao ya awali.Hii hupelekea mashuleni kuwepo na walimu wasio na nia,yani bora liende,yani amekuwa mwalimu kwa sababu ilibidi.Hili liko wazi kabisa kwani waalimu wengi wameshajiendeleza na wengi wameshakuwa wahasibu,wanasheria na kadhalika.


Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hata jamii inaunga mkono hali hii.Mtoto anaweza kuwa na malengo ya kuwa mwalimu,lkn anapofika form six na akifaulu vizuri ,mathalani division one,na akiwaambia wazazi kuwa ana mpango wa kujiunga na vyuo vya ualimu, wazazi utashangaa kuwa wanamwambia mtoto wao kuwa anapotea njia.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya waalimu hawafikirii ni kwa namna gani wataongeza ufanisi ktk kufundisha bali huwa wanafikiri ni kwa namna gani wataachana na kazi hii.Jambo hili ni lakawaida kabisa kwa kizazi cha sasa tofauti kabisa na zamani ambapo ualimu ulikuwa ni wito.

Hali hii nitatizo kubwa sana ktk sekta ya elimu.

Hivi ni kwa namna gani hali hii itatokomezwa?

Je,hali hii inaathari zipi kwa wanafunzi?

"Nina ndoto ya kwamba itafika wakati nafasi za ualimu zitapiganiwa na hapo ndipo waalimu wa kweli wataanza kupatikana na elimu ya kweli itaanza kutolewa"

Comments

Ronald Reagan aliwahi kusema kuwa "wale wote wanaopigania hakiza utoaji mimba wameshazaliwa". Ndio tunayoona hapa Kaka. Wale wote wanaopinga wana wao kuwa waalimu ni wale ambao "wameelimika". Sasa hawaoni thamani ya ualimu. Yaani ni wale wanaovunja daraja wakishamaliza kuvuka ama wanafukia kisima wamalizapo kuchota maji. Wanasahau leo na kesjo.
Kama ulivyosema Mkuu ni kwamba ualimu umekuwa kama "kishikizo" cha wale wanaofikiria nini cha kufanya baadae.
Inasikitisha kuona si wito tena. Ni kama uuguzi hapa Marekani. Watu na ujuzi, sifa na hiba za kuwa walivyo wanabadili kazi ili kuwa wauguzi kwa kuwa tu unalipa. Matokeo yake wengi wanayaona maana hakuna anayefunza kukinga, ni kufanya alichokaririshwa tu juu ya nini cha kutibu kwa ktumia nini.
Athari za kukosekana kwa wito wa ualimu nyumbani ni nyingi na twaona kuwa hata njia za ufundishaji wa sasa ni "ili afaulu" na si aelewe afundishwacho.
Natumai ndoto ulizonazo zitatimia, lakini si kwa malengo na mipango iliyopo serikalini.
Amani Kwako Kaka.
Daima pamoja
Albert Kissima said…
Kweli kaka Mubelwa ndoto hiyo serikalini haipo kwa sasa lakini naamini ipo siku! ipo siku tutapata viongozi wa kweli watakaowajali walimu ambapo nafasi hizo zitatafutwa kama lulu na itabidi vigezo vizingatiwe japokuwa watakuwepo wale watakaotumia njia ambazo si halali.
Anonymous said…
Ualimu unapuuzwa kwa sababa jamii haina haja na maarifa. Yawasaidie nini?

Jamii inaota ndoto za 'mihela' ndio maana ufisadi ni kazi inayolipa nchini.

Huwezi kuzungumzia watu kujielewa kama hawana habari na maarifa. Zungumzia namna ya kutengeneza 'fweza' uone utakavyoonekana lulu.

Tumepotea njia ingawa hatujui.

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?