Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili
Mambo makuu ya kuzingatia ili kufanikisha upimaji endelevu wenye tija. Picha: Mwandishi wa Makala. Hakuna mjadala kuwa upimaji endelevu ni sehemu muhimu sana wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Taarifa za namna ufundishaji na ujifunzaji unavyokwenda zinategemewa kupatikana kupitia upimaji endelevu bora. Makala haya yanalenga kuendelea kujadili mambo makuu manne kama tulivyoyaona katika makala iliyotangulia. Mambo hayo ni ufafanuzi wa kina wa mambo makuu yanayopaswa kujifunzwa na wanafunzi (clarifying learning), kuwajengea wanafunzi ari ya kujifunza (activating learners), kutoa mrejesho wa maendeleo yao (providing feedback) na kutafuta ushahidi wa ujifunzaji (eliciting evidence of learning). Katika makala haya nitajadili utoaji wa mrejesho wa Shughuli za Ujifunzaji (providing feedback) na utafutaji wa ushahidi wa ujifunzaji (Eliciting evidence of learning). Kutoa Mrejesho wa Shughuli za Wanafunzi (Providing Feedback) Kila anachokifanya mwanafunzi, anatamani sana ...