Njia Nne za Kutumia Ufundishaji na Ujifunzaji Unaomzingatia Mwanafunzi
Wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Mpwapwa wakishiriki kwenye moja ya shughuli za ujifunzaji darasani. Picha na Mwandishi wa Makala haya. Katika Makala zilizotangualia, nimekuwa nikijadili kuhusu elimu inayomzingatia mwanfunzi, hususani ujifunzaji wa kiudadisi. Makala ya kwanza ilijadili kuhusu maana, faida na namna ujifunzaji wa kiudadisi unavyoweza kutumiwa mashuleni. Makala ya pili ililenga kujadili mbinu zinazoweza kutumiwa kujenga utamaduni wa ufundishaji na ujifunzaji wa kiudadisi mashuleni. Makala ya tatu kwa upande mwingine, ilijadili namna mfumo wa sasa wa ufundishaji mashuleni unavyowanufaisha walimu kuliko wanafunzi. Makala haya yanalenga kujadili njia nne ambazo walimu na wawezeshaji wengine wanaweza kuzizingatia ili kuwezesha kwa kufuata misingi ya ujifunzaji wa kiudadisi. Njia hizi zitakazojadiliwa kwa kina ni Kuwamilikisha somo wanafunzi, mwalimu kuongea kwa kiasi na kuuliza maswali zaidi, kusisitiza uthibitisho wa hoja za wanafunzi na mwalimu...