Singida: Wananchi Wakubali Malazi Bora Katika Bora Mazingira-Sehemu ya Pili.
Sehemu ya kwanza ya makala hii ilitazama kwa ujumla harakati za wakazi wa Singida hususani katika wilaya ya Iramba wanavyojitahidi kujenga makazi bora kwa kutumia matofali ya kuchoma na kuachana na nyumba za asili aina ya tembe. Katika wilaya ya Iramba, ujenzi wa makazi bora umekuwa na athari kubwa sana katika mazingira kutokana na ukweli kuwa, uandaaji wa matofali unahusisha uharibifu mkubwa wa mazingira. Mbali na uharibifu mkubwa wa misitu unaotokana na kukata miti ili kupata kuni za kuchomea matofali, lakini pia kwa bahati mbaya sana tabaka la juu la udongo ndilo ambalo hutumiwa katika kuandaa matofali. Uharibifu huu umepelekea maeneo mengi kuwa na mashimo yanayosababisha mmomonyoko wa udongo na pia wananchi kushuhudia mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotarajiwa. Nilipata bahati ya kutembelea moja ya msitu wa asili ulioko katika kijiji cha Kyalosangi kata ya Kinampanda wilayani Iramba na kushuhudia uharibifu mkubwa wa msitu huu. Picha hapa chini inaonesha angalao mandhari nz...