Singida: Wananchi Wakubali Malazi Bora katika Bora Mazingira-Sehemu ya Kwanza
Nyumba ya asili ya wakazi wa Mkoani Singida, maarufu kwa jina la "Tembe" Bila shaka umewahi kuzisikia ama kuziona nyumba zinazoezekwa kwa kutumia udongo badala ya bati almaarufu kama “tembe”. Nyumba hizi zinapatikana kwa wingi katika mkoa wa Singida na hata katika mikoa mingine kama vile Dodoma. Nyumba hizi za tembe ni za kiasili kwa mkoa huu wa Singida. Hadi sasa nyumba hizi bado zinatumika kwa kiasi kikubwa tu kama nyumba kwa ajili ya malazi ya wakazi wa mkoa huu. Miaka ya hivi karibuni, wakazi wa mkoani Singida wameanza kujenga nyumba zilizo bora zaidi. Wakazi hawa wamejikita katika ujenzi wa nyumba za kuishi kwa kutumia matofali ya kuchoma. Taratibu wanaachana na ujenzi wa nyumba za tembe pamoja na kuwa, kwa kiasi fulani, katika ujenzi wa makazi haya bora, wamekuwa wakihamishia namna fulani ya ujenzi unaoshabihiana na ule wa nyumba za tembe. Mfano, nyumba za tembe huwa zinakuwa na vidirisha vidogo vidogo. Zipo pia baadhi ya nyumba bora zilizojengwa kwa matofa...