Tanzania Iliyobarikiwa Isiyo ya Wabarikiwa
Picha ya Muonekano wa Kaldera ya Ngorongoro Tanzania inajulikana kuwa na rasilimali nyingi sana ambazo kama zingetumika vizuri, basi watanzania tungekuwa katika hali nafuu sana ya maisha kuliko hivi sasa. sitamani kuwakumbusha utajiri ambao nchi ya Tanzania ilionao kwani umeshakuwa ni wimbo ambao kwa sasa pengine hakuna tena anayetaka kuusikiliza kabisa. Kama nilivyotangulia kusema katika bandiko lililopita, nilipata fursa ya kutembelea maeneo mengi ya mkoa wa Singida, hususani wilaya ya Iramba. nilisema pia, kuna mengi niliyojifunza kwa kusimuliwa na kwa kujionea mwenyewe. leo nitawajuza kuhusu mgodi mpya wa dhahabu nilioushuhudia katika ukanda wa bonde la ufa la sekenke katika eneo liitwalo Mgongo. Mgodi wa Mgongo uko wilaya ya Iramba-sekenke, kama mita mia mbili kutoka ilipo shule ya msingi Mgongo; shule ambayo ndiyo niliyofikia kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya waalimu walio katika mafunzo ya muda mrefu ya kufundisha. Nilifika hapo tarehe 07/03/2012 na nilipewa taarif...