Posts

Showing posts from January, 2011

Uchawi unahitaji vita kama ya ukeketaji wa Wanawake!

Ukeketaji wa wanawake nchini Tanzania ni jambo ambalo (pengine na kwingineko duniani) kwa miaka iliyopita lilikuwa limeshamiri sana katika jamii zetu kiasi kwamba watu pengine hawakukaa kuwaza kuwa ipo siku jambo hili litapewa kipau mbele kwa kupingwa na wanaharakati duniani kote. Hili limefanyika na sasa jamii kwa kiasi kikubwa imekuwa adui wa jambo hili na kwa miaka ya hivi karibuni ukeketaji umepungua kwa kiasi kikubwa.

Wahusika wa ukeketaji wamejisalimisha, wamesaliti amri kwa wingi wao japokuwa bado wapo pia ambao wanaendelea na ukeketaji.

Uchawi kama ukeketaji ulivyokuwa, ni tatizo kwa Taifa letu watanzania. Sehemu nyingi za Tanzania zinakosa maendeleo ambapo, pamoja na mambo mengine, uchawi unachangia sana.

Ni siku za hivi karibuni tumesikia huko Mbozi mkoani Mbeya, walimu walizikimbia shule walizokuwa wanafundisha kwa madai ya kusumbuliwa na mambo ya kichawi. Si Mbeya tu, hali hizi zipo sehemu nyingi Tanzania.

Si walimu tu wanaathirika, lakini mambo mengine mengi ya kimaendeleo…