Posts

Showing posts from October, 2010

Mashaka katika kituo cha kupigia kura cha Siuyu namba mbili chenye namba 00014472 jimbo la Singida Mashariki.

Kituo hiki kinahisiwa kuwa, mawakala wawili wa Chadema ambao pia walitiliwa mashaka na wanachama wa chama hiki wakati wa kuapishwa, ni wafuasi wakubwa wa chama tawala. Tetesi zinazidi kudokeza kuwa mawakala hawa ni washirika wakubwa wa mgombea mmoja wa chama cha mapinduzi (CCM), na inasadikiwa kuwa wamepandikizwa kwenye uwakala wa chadema ili kufanikisha uchakachuaji wa kura pale inapobidi.

Ukaribu huu wa mawakala hawa wa Chadema na mgombea huyu wa CCM ndio hasa unaoelezwa kuleta kujiuliza kwingi na kuwafanya wazungumzaji kuwa na hofu juu ya kura za wagombea wa chama chao kutokuwa katika hali ya usalama.

Wito wangu ni kuwa, yasemwayo yapo na kama hayapo, yaja. Uangalizi makini bado wahitajika. Kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuhakikisha kuwa haki yake haipindishwi. Kama kweli hali hii ipo, bila shaka si kwenye kituo kimoja tu, bali yawezekana ni vituo vingi, na hili laweza kugharimu vyama vya upinzani, hususani Chadema.

Nitazidi kutoa taarifa kwa kadiri ya inavyowezekana, japoku…

Mchakato wa kuapishwa kwa mawakala Jimbo la Singida Mashariki-Uchakachuaji ukatishao tamaa

Jana nilikuwa kwenye mchakato wa kuapishwa kwa mawakala watakaosimamia na kuangalia kura za wagombea ili zisiende kusikokusudiwa na kusiko kwa matakwa ya wapiga kura.

Shughuli hii ilifanyikia katika shule ya Msingi Makiungu. Mbali na zoezi hili, pia kulikuwa na semina kwa ajili ya wasimamizi wa uchaguzi.

Zoezi hili la kuapishwa kwa mawakala halikwenda vizuri hata kidogo. Mchakato huu ulikuwa na dosari mbalimbali na ambazo kwa kiasi kikubwa zitakuwa na adhari sana kwa vyama vya upinzani na hasa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)

Majina mengi ya watu waliojitolea kuwa mawakala wa vyama walijikuta wakikosa nafasi hizo na badala yake kuchukuliwa na watu wengine bila hata kuwa na sababu za kueleweka.

Kwa mujibu wa wananchi wanasema kuwa majina ya watu waliotakiwa kuapishwa ni yale yaliyotolewa na ofisi ya tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya ambayo yaliwasilishwa na wagombea wa vyama husika.

Kasoro nyingine iliyojitokeza ni ile ya mtu mmoja kuwa wakala wa vyama viwili kwa wakati mmoja wakat…

Nipo Singida

Kati ya vitu nivipendavyo katika maisha ni kusafiri, hususani kutembelea sehemu ambazo ni ngeni machoni mwangu. Pamoja na sababu nyingine muhimu, hili nalo limekuwa miongoni mwa sababu zinifanyazo kwa sasa nirindime nikiwa hapa Singida.

Nipo kijijini Siuyu. Ni mbali kidogo na Singida Mjini. Nauli ya kwenda na kurudi ni shilingi za kitanzania Elfu nne. Ni pesa nyingi hizi, kwa kuzingatia hali halisi ya asilimia kubwa ya wakazi. Barabara iunganishayo mji na kijiji hiki pamoja na vya jirani haipo katika kiwango cha lami, si nzuri ya kuridhisha, hivyo magari ya abiria ni machache.
Kwa kuzingatia uchache wa magari yapitayo katika barabara hii, magari hayo pamoja na kuchukua abiria, lakini pia yamekuwa yakibeba hata mizigo mingine kama nondo, mbao, mabati n.k Hakika swala la usafiri katika kijiji hiki na vijiji jirani kama Unyamikumbi, Ughaugha, Ngaghe na Unyaghumpi pamoja na vijiji vingine bado ni tatizo kubwa. Gari la abiria laweza kusubiriwa hata kwa zaidi ya masaa mawili hadi matatu.

He…