Posts

Showing posts from July, 2010

Tunazingatia matumizi ya Lazima na Hiari kwa pato letu?

Ni mda mrefu ulipita sikuonekana katika ulimwengu huu wa ku-blogu. Nilibanwa na baadhi ya majukumu, na sasa nimerudi tena na tupo pamoja. Niombe radhi kwa kutokuweka wazi juu ya adimiko langu. Naam, wakati wa adimiko, nilipata kujifunza mengi, na leo naona ni vema nigusie kidogo matumizi ya pato la mtanzania mmoja mmoja na mchango wake katika kuendeleza wimbi la umasikini au kuweza kujikwamua na umasikini. Popote pale Tanzania, mjini na vijijini, asilimia kubwa ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi huonekana katika pilikapilika za hapa na pale. Wapo wafanyao kazi halali na wale wasiofanya kazi halali, lakini mwisho wa siku kila mmoja anapata ujira wake. Wapo waliojiajiri na pia walioajiriwa. Waliojiajiri, mwisho wa siku huweka chao kibindoni na wale walioajiriwa husubiri mwisho wa mwezi ndipo waweke chao kibindoni. Maisha haya humgusa yeyote yule ambaye si tegemezi katika familia au sehemu aishiyo. Huko mijini, watu huonekana kila mmoja na pilika yake ilimradi mkono uingie ki...

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?